Naomba msaada wa kisheria nduguzangu:

sosholeza

New Member
Joined
Jan 27, 2013
Posts
1
Reaction score
1
Mume wangu ameniacha baada ya kupata mwanamke mwingine. Kwa miaka 17 tulifanikiwa kujenga nyumba 2 na kagari ka 1. Hivi sasa nyumbani haji tena amehamia kwenye nyumba yetu ya pili na huyo mwanamke. Mimi nimebaki na watoto wangu wawili kwenye nyumba ya awali pamoja na mali nyingine.

Nimejaribu kuongea naye hata na ndugu na viongozi wa dini ila imeshindikana hataki kurudi. Amesema nyumba nichukue pamoja na vyote vilivomo, nami nimeridhia maana sina jinsi.

Ombi langu kwenu wana JF ni kutaka kujua wapi pa kuanzia kumiliki hyo nyumba maana haina hati. Ahsanteni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…