Naomba msaada wa kisheria: Nimepandishwa cheo ila bado mshahara wa zamani

Naomba msaada wa kisheria: Nimepandishwa cheo ila bado mshahara wa zamani

inchaji

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2019
Posts
2,427
Reaction score
4,944
Heshima kwenu wakuu.

Naomba ushauri wa kisheria. Ninafanya kazi kampuni binafsi. hawa wanaoitwa wawekezaji.

Mwaka 2018, miezi kama 18 iliyopita nilipandishwa cheo.Cha ajabu nimeendelea kulipwa mshahara uleule wa cheo cha zamani na kila nikimuambiwa muajiri wangu anachukulia poapoa.

Vilevile salary slip zangu zimekuwa zikija na details zenye cheo changu cha zamani lakini nikiuliza kwa nini inakuwa vile napewa majibu ya juu juu kuwa watabadilisha kwenye payroll lakini mpaka sasa hawajafanya hivyo.

Kwa nafasi niliopo sasa natakiwa nilipwe mara mbili ya nilichokuwa nikipata zamani baada ya makato. kumbukumbu zipo ambazo zinaonesha wapo wenzangu wanaofanya nafasi ileile wanalipwa mara mbili zaidi yangu. Vilevile nafasi niliyopo nilirithi kwa mtu aliejiuzulu na alikuwa akilipwa mara mbili ya ninacholipwa mimi.

Nimfanyeje huyu muajiri?
 
fuatilia wakuambie issue yako nani anaifanyia kazi then ukomae nae
 
Back
Top Bottom