Kwani mkataba wenu unasemaje kuhusu notice za kuhama au kusitisha mkataba? Vinginevyo kama mkataba wa miezi mitatu upo ni sharti umalize kodi yako vinginevyo anatakiwa kurejesha kodi with penalty only if and only if mliandikiana hivyo. Pia pengine mkataba unasema kama umeleta ukorofi kwa wapangaji au mwenye nyumba basi unaondolea haraka. Ni lazima kuwe na tatizo, si rahisi akupe tu notisi uondoke. Nenda kashitaki serikali za mtaa au mjumbe ili muweke mambo sana kulingana na mkataba wako ndipo kama ukishindwa unaweza kusonga mbele kumshtaki. Na unapata zuio la kuhama haraka. Ila wakuu, kuwa na makazi yako binafsi ni raha kupita raha zote hata kama utalia uji wa chumvi ndani yake. Kazana siku moja utakuwa na kwako.