LULAMSO
Member
- Apr 26, 2013
- 56
- 9
Mimi ni mfanyabishara wa bidhaa ndogo ndogo dukani. Siku chache zilizopita kuna mteja alikuja dukani kwangu kupata huduma, baada ya kumhudumia alinilipa pesa ambayo kwa bahati mbaya sikuwa na chenji yake hivyo nililazimika kumuacha dukani kwangu na kwenda duka la jirani kutafta chenji. Wakati huo yeye nillimuacha dukan kwangu kwa mda nikiwa na imani kuwa angeniangalizia kwa mda ili nitafte chenji. Lakini kabla sijaanza harakati hizo za kumtaftia chenji simu yake na yangu niliziweka mezani kwangu kuna kitu nilikuwa najifunza kutoka kwenye simu yake kama ilivyo kawaida kushangaa technolojia mpya.
Dakika chache baadae narejea kumkabidhi chenji yake nilikutana nae mlangoni akiwa tayari kuondoka. Sikuwa na chakuhofu, nilimkabidhi chenji yake sikukumbuka chochote kuhusu simu. Dakika chache baadae nikakumbuka kuhusu simu yangu maana kuna mtu nilitaka kumpigia. Wakati huo hakuna mtu mwingine yeyote alieingia dukan kwangu tangu atoke yeye. Namuuliza anakataa, nawezaje kumdhibiti mtu huyu kisheria? Naomba msaada wenu tafadhari.
NB: Kinachoniuma simu yangu ni ya hela nyigi sana, ni ya laini mbili. na kuna pesa kibao ndani yake, nifanyeje?