Naomba msaada wa kupata mwanasheria bora ili anisamamie kuandika wosia.....

bakuza

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2010
Posts
492
Reaction score
104
Naomba kusaidiwa kupata mwanasheria mzuri ili nikaandike wosia wangu. Nadhani inaeleweka ni jambo jema kuandika wosia mapema ili baadaye kusiwe na usumbufu kwa watoto na familia. Pia naomba kufahamishwa utaratibu wa kuandika wosia kwa mwanasheria.

Naomba anayejua basi anijulishe ama kwa PM ama kupitia Email: bakuzab@yahoo.com.

Natashukuru kwa ushirikiano wenu.
 
umefanya uamuzi mzuri sana kutaka kuandika wosia. nakushauri, pamoja na kutafuta mwanasheria akusaidie, bofya hapa SHERIA KWA KISWAHILI pia tafuta kitabu kifuatacho kitakusaidia.

View attachment 104671

View attachment 104672View attachment 104672
 
mwanasheria yoyote anaweza kuandika wosia, hakuna ufundi wa kutofautiana ubora katika kuandika wosia, mpka useme huyu ni mzuri na huyu ni mbaya, cha msingi sana ni kufanya kitu kinaitwa estate planning, kupangilia mali zako, na watu unaotaka kuwarithisha kabla ya kuandika wosia. Orodhesha mali zako zote, mf. zipo wapi, thamani yake, unataka kumpatia nani, nani awe msimamizi wa mirathi, uwe na mashahidi wasiopungua wanne, wawili nje ya familia na wawili ndani ya familia, then mpelekee mwanasheria yoyote atakuandikia
 


Asante Stroke hii imekaa vizuri mkuu...nimepata ufahamu mkubwa kaka.Ila kusema mwanasheria bora nilimaanisha asiwe miongoni mwa wale wasio na usajiri ama waliochakachua fani.
 
kwa kuongezea, kwenye kitabu hicho, nimeandika aina zote za wosia, namna ya kuandika wosia sahihi, masharti yake kwa wosia wa maandishi (hata ule wa mdomo) kama vile uwe na mashahidi wangapi na ambao wako vipi, mahali pakutunza wosia na mambo yote kuhusu wosia na ugawaji mirathi. you will really like it. hata hivyo, kama ukikisoma kitabu hiki chote, utakuwa kwenye nafasi ya kuandika wosia wewe mwenyewe bila hata kwenda kwa mwanasheria, kimeandikwa kwa kiswahili. bofya hapa SHERIA KWA KISWAHILI au angalia post yangu hapo juu.
 
umefanya jambo jema mkuu kwa kuwaandalia maisha mema watoto wako.
 
asante mkuu Mishpacha
 

Sasa mdau kazi za wanasheria wakiachiwa watu wengine inakuwa professional trespass ebu mwache atafute wanasheria tumuandikie, na hiyo ndio Specialization , ni sawa anakuja mgonjwa wa malaria kwa daktari, daktari anampa kitabu cha kujifunza kujitibu malaria, ka ni hivyo ni ni maana ya kuwa na wanasheria au professionals zingine.
 
sawa kiongozi, nafikiri utakuwa umejua kwanini nimemwambia atafute kitabu hicho, nilitaka aniungishe kitabu. ila nilishamwambia awatafute wanasheria pia.
 
sawa kiongozi, nafikiri utakuwa umejua kwanini nimemwambia atafute kitabu hicho, nilitaka aniungishe kitabu. ila nilishamwambia awatafute wanasheria pia.
Hapo sasa mdau nimekusoma ka swala ni kukunga kwenye kununua vitabu sina pingamizi nalo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…