Naomba msaada wa kusafisha taa za gari

profesawaaganojipya

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2015
Posts
1,595
Reaction score
3,416
wadau naombeni msaada,namna ya kusafisha taa za mbele,kubwa za gari,jana usiku nimepata shida sana barabarani,mwanga ulikuwa mdogo na hafifu sana,alafu taa ya kushoto ina mwanga mkali kishinda ya kulia,msaada please..
 
Njia rahisi ya kwanza. Chukua collate changanya na maji. Paka kwenye kioo. Acha muda fulani safisha. Inasaidia kidogo.
 
Unaishi pori gani? Mbona ukipark sehemu yoyote mjini vijana wanakuja kuomba kusafisha na madawa yao?
 
Njia rahisi ya kwanza. Chukua collate changanya na maji. Paka kwenye kioo. Acha muda fulani safisha. Inasaidia kidogo.
Naamini ulimaanisha Colgate. Ni kweli. Inasaidia.
 
Hao hapo.
Hii huduma inafanywa sikuhizi kila sehemu hata huku mitaa ya gerezani kuna jamaa alisafisha taa zangu Kwa TSH 20000...
Inasaidia Ila baada ya miezi 3 Hali ya ukungu inarudi tena kama zamani yaani ni magumashi Tu.
Fundi wangu alinishauri zifunguliwe taa zote ili zisafishwe Kwa njia ya kawaida
 
Ukishasafisha weka sticker za taa, zinasaidia ukungu kutorudi. Maeneo ya kumumba hapo wanafanya bei haizidi 30,000 kwa taa zote 2
 
Ukishasafisha weka sticker za taa, zinasaidia ukungu kutorudi. Maeneo ya kumumba hapo wanafanya bei haizidi 30,000 kwa taa zote 2
Jamaa aliniambia hicho kitu Ila nikapuuza.
Ngoja nikisafisha tena nitaweka hizo stika
 
Ukishasafisha weka sticker za taa, zinasaidia ukungu kutorudi. Maeneo ya kumumba hapo wanafanya bei haizidi 30,000 kwa taa zote 2
Sticker za taa ndo zipoje?
 
Sticker za taa ndo zipoje?
sijui nikuelezeje kirahisi ila ni sticker zinakuwa clear, nyingine zinakuwa na rangi blue kwa mbali, na nyingine smoked. Wanabandika juu ya taa kama wanavyobandika tint. Clear ni nzuri kwa sababu haiathiri nguvu ya mwanga wa taa na mtu hawezi kujua kama umebandika kitu. Za blue zianonyesha kidogo ila pia zinapendeza, na haziathiri mwanga pia kama zile smoked
 
Nimeagiza hii kitu, nitakuwa nafanyà hii kazi mwenyewe... weekends are for home chores!
 
Nauza mashine ya kusafisha taa za gari kwa bei nafuu ni mpya na ya kusasa kabisa unaweza kuitumia kwa matumizi yako binafsi na kwa biashara pia kwa shilingi 250,000/= maongezi pia yapo
Kwa mawasiliano NO 0659645794 AU TSAP NO 0628462722View attachment 2456560
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…