Naomba msaada wa mawazo (kisheria) ktk hili lifuatalo

Mawazo huru

Member
Joined
Jul 7, 2011
Posts
13
Reaction score
1
Nina mama yangu kijijini ambaye alikuwa na ardhi yake nusu heka sasa ikatokea tetesi kwamba tigo wanataka jenga mnara pale, baada ya muda kwel wakaja jamaa ila wakasema wanataka ile ardh kwa ajili ya kujengea ofisi mama akawaambia nasikia mnajenga mnara na mm nitawauzia kama wajenga mnara, wakakataa hawatajenga mnara wakamdanganya mpaka yule mama akawauzia kwa milion 3 ndani kuna msingi wa nyumba na miti. Sasa baada ya muda kidogo wameanza jenga mnara wa tigo. Je hapo kisheria naweza fanya lolote kumusaidia mama yangu
 
Imekula kwake, lakini fatilia ujiridhishe, isijekuwa wamekula hela zaidi huyo mama wakampa hizo.

Kisheria unaweza kuwageuzia kibao kama utapata wakili mzuri ataeweza kuikinaisha mahakama kuwa mama alichukuwa maamuzi kwa kurubuniwa, uzee, hana akili timamu, na ikiwa sehemu hiyo viwanja vina thamani zaidi ya hiyo waliotoa kwa wakati huo.
 
Wewe ulikuwa wapi mpaka ukamwacha Mama wakamrubuni? Keshauza basi Sio Mali Yale tena, they can do what they want, wanaeeza jenga chochote.
 
Nilikuwa shule, ila mama zetu vijijin hawana mtu wa wasaidia wamemdanganya mama yangu sasa yupo hoi kwa masononeko, nataman nijue how ya kudili na hawa matapeli nakosa usingizi kabisa mpaka nitakapofanya chochote nia ninayo ila sijui sheria na walichofanya ndio ile mikataba ya mangungo.
 
Imekula kwake, lakini fatilia ujiridhishe, isijekuwa wamekula hela zaidi huyo mama wakampa hizo.

Kisheria unaweza kuwageuzia kibao kama utapata wakili mzuri ataeweza kuikinaisha mahakama kuwa mama alichukuwa maamuzi kwa kurubuniwa, uzee, hana akili timamu, na ikiwa sehemu hiyo viwanja vina thamani zaidi ya hiyo waliotoa kwa wakati huo.
Nawasiwasi kuwa kuna matapeli ktk timu zinazotafuta maeneo ya kuweka minara kiasi kwamba wakijua wapi wanatakiwa waweke huo mnara wanaanza kuimiliki ardhi wao. Walisema mbele ya mashahidi kuwa watajenga ofisi ila wakajenga mnara baadaye, ninachojua kuwa hii tabia hawajaanzia kwa mama yangu walisha mtapeli mzee kijiji jilani kwa njia ileile.
 
Kwa vile miradi hii ya kijambazi ya makampuni ya simu ina mkono wa wakubwa haki haitatendeka. Mama yako ana kesi nzuri kama kungekuwa na mfumo mzuri wa haki isiyohitaji mfuko bali ukweli. Hapa hata akitumia dhana ya mistake of fact anatosha kupata kinga achia mbali kuangalia welewa wa walioingia naye mkataba kulinganisha na wa mama yako. Kimsingi hata kujenga mnara wa simu kwenye eneo la makazi ni kosa sema kwetu ni kwa vile tuna watawala wanaowauza watu wao. Katika nchi za magharibi huwezi kuona mnara kwenye makazi ya watu kwa vile ina mionzi yenye madhara makubwa kwa afya ya viumbe vilivyo hai. Kuna siku Tanzania italipuka na kansa kutokana na kuzagaa kwa minara ya simu. HEBU SOMA HAPA KWA MAELEZO ZAIDI.
 
Unataka kumsaidia nini mama yako? Kuwa aongezewe hela kwa sababu hawajengi ofisi ama hutaki akae karibu na mnara?
Sina hakika, ila sidhani kama una nguvu juu ya wanachofanya na ardhi waliyonunua. Kama hofu yako ni usalama wa mnara wasiliana na NEMC, japo kisheria as long as kuna mita 6+ kati yenu na mnara hakuna kosa.
 
mikataba ya kuuziana inaweza kumsaidia japo naamini watakuwa wameandika wanananua eneo sidhani kama wameelezea watalifanyia nini ila kama wameelezea inaweza kusaidia .. itabidi kuwaona wanasheria au kwenda ardhi kupata ushauri zaidi
 
Pole sana. Eneo liko wapi?
 
mikataba ya kuuziana inaweza kumsaidia japo naamini watakuwa wameandika wanananua eneo sidhani kama wameelezea watalifanyia nini ila kama wameelezea inaweza kusaidia .. itabidi kuwaona wanasheria au kwenda ardhi kupata ushauri zaidi

Tatizo elimu, mama yangu darasa la saba enzi za mwalimu ngoja nitamuuliza kama hata mkataba wa mauziano anao.
 
Kilombero na Kilosa kuna jamaa wa Morogoro ndo wanafanya hizo dili. Nimeona cases mbaya zaidi ya hiyo. Sidhani kama unaweza kufanya lolote, mnara ukishajengwa unaweza kulalamika endapo kuna usumbufu. Kuna mama kilosa mabehewa walimuingiza mjini akawauzia laki 2, it was 2008! Wakasema wanajenga mashine ya kukoboa mpunga. Mwisho wa siku iliamriwa waondoke kwa sababu ya tank kubwa la petrol, ukaribu na nyumba na kelele za generator. Sijui kama waliondoka!
Mpige mkwala mama yako, wewe umeshakuwa mkubwa na umesoma. Asifanye maamuzi bila kukushirikisha. Next atakuambia kauza hapo anapoishi!
 
Unataka kumsaidia nini mama yako? Kuwa aongezewe hela kwa sababu hawajengi ofisi ama hutaki akae karibu na mnara?
Sina hakika, ila sidhani kama una nguvu juu ya wanachofanya na ardhi waliyonunua. Kama hofu yako ni usalama wa mnara wasiliana na NEMC, japo kisheria as long as kuna mita 6+ kati yenu na mnara hakuna kosa.

Hofu yangu sio madhara ya mnara kwani anaishi mbali na kiwanja hicho. Hofu yangu ipo kwenye utapeli ambao naona wa makusudi kwamba kuna watu ktk kampuni la simu husika wanajua kwamba eneo hili tutajenga mnara wanatangulia kumrubuni mmiliki mapema kwa kununua eneo kwa gharama ndogo sana baada ya hapo wao ndio wanaingia mkataba na kampuni husika na hawa lazima wanakuwa na uhusiano na mamlaka ikibidi ni waajiriwa
 
ni PM nitakueleza cha kufanya. hakikisha una yale makaratasi yote aliyopewa na hao jamaa..........vile vile hakikisha yana sahihi, tarehe na mihuri yote. I don't need payment from you guy I will show you the entrance door.
 
Bary nasubili kwa hamu ushauri wako nachotaka kufanya sio kutafuta haki kwa mama yangu tu nitahakikisha nalitangaza tatizo na kuwa haibisha hawa matapeli. Naomba mungu anitangulie na kunilinda.
 
Kilombero na Kilosa kuna jamaa wa Morogoro ndo wanafanya hizo dili. Nimeona cases mbaya zaidi ya hiyo. Sidhani kama unaweza kufanya lolote, mnara ukishajengwa unaweza kulalamika endapo kuna usumbufu. Kuna mama kilosa mabehewa walimuingiza mjini akawauzia laki 2, it was 2008! Wakasema wanajenga mashine ya kukoboa mpunga. Mwisho wa siku iliamriwa waondoke kwa sababu ya tank kubwa la petrol, ukaribu na nyumba na kelele za generator. Sijui kama waliondoka!
Mpige mkwala mama yako, wewe umeshakuwa mkubwa na umesoma. Asifanye maamuzi bila kukushirikisha. Next atakuambia kauza hapo anapoishi!

kaka nasikia kidogo basi kunamzee aliwauzia kwa laki tatu. Tuungane watanzania kupinga hii aina ya ujambazi leo mama yangu kesho wazazi wako, watoto wako ukiwa umekufa huu ndio muda muhafaka wa kupigana vita hii.
 
Tatizo elimu, mama yangu darasa la saba enzi za mwalimu ngoja nitamuuliza kama hata mkataba wa mauziano anao.

lakini walikosekana baadhi ya ndugu kujaribu kutoa msaada wakati wa makubaliano?
 
mimi naona anaweza kwenda mahakaman na kudai haki yake na kuraise objection that aliingia kwenye mkataba kwa kudanganywa(fraud) coz wao c walmwambia hawajeng mnara lakn matokeo yake wamejenga
 
Back
Top Bottom