Mawazo huru
Member
- Jul 7, 2011
- 13
- 1
Wewe ulikuwa wapi mpaka ukamwacha Mama wakamrubuni? Keshauza basi Sio Mali Yale tena, they can do what they want, wanaeeza jenga chochote.
Nawasiwasi kuwa kuna matapeli ktk timu zinazotafuta maeneo ya kuweka minara kiasi kwamba wakijua wapi wanatakiwa waweke huo mnara wanaanza kuimiliki ardhi wao. Walisema mbele ya mashahidi kuwa watajenga ofisi ila wakajenga mnara baadaye, ninachojua kuwa hii tabia hawajaanzia kwa mama yangu walisha mtapeli mzee kijiji jilani kwa njia ileile.Imekula kwake, lakini fatilia ujiridhishe, isijekuwa wamekula hela zaidi huyo mama wakampa hizo.
Kisheria unaweza kuwageuzia kibao kama utapata wakili mzuri ataeweza kuikinaisha mahakama kuwa mama alichukuwa maamuzi kwa kurubuniwa, uzee, hana akili timamu, na ikiwa sehemu hiyo viwanja vina thamani zaidi ya hiyo waliotoa kwa wakati huo.
mikataba ya kuuziana inaweza kumsaidia japo naamini watakuwa wameandika wanananua eneo sidhani kama wameelezea watalifanyia nini ila kama wameelezea inaweza kusaidia .. itabidi kuwaona wanasheria au kwenda ardhi kupata ushauri zaidi
Pole sana. Eneo liko wapi?
mikataba ya kuuziana inaweza kumsaidia japo naamini watakuwa wameandika wanananua eneo sidhani kama wameelezea watalifanyia nini ila kama wameelezea inaweza kusaidia .. itabidi kuwaona wanasheria au kwenda ardhi kupata ushauri zaidi
Unataka kumsaidia nini mama yako? Kuwa aongezewe hela kwa sababu hawajengi ofisi ama hutaki akae karibu na mnara?
Sina hakika, ila sidhani kama una nguvu juu ya wanachofanya na ardhi waliyonunua. Kama hofu yako ni usalama wa mnara wasiliana na NEMC, japo kisheria as long as kuna mita 6+ kati yenu na mnara hakuna kosa.
ni PM nitakueleza cha kufanya. hakikisha una yale makaratasi yote aliyopewa na hao jamaa..........vile vile hakikisha yana sahihi, tarehe na mihuri yote. I don't need payment from you guy I will show you the entrance door.
Kilombero na Kilosa kuna jamaa wa Morogoro ndo wanafanya hizo dili. Nimeona cases mbaya zaidi ya hiyo. Sidhani kama unaweza kufanya lolote, mnara ukishajengwa unaweza kulalamika endapo kuna usumbufu. Kuna mama kilosa mabehewa walimuingiza mjini akawauzia laki 2, it was 2008! Wakasema wanajenga mashine ya kukoboa mpunga. Mwisho wa siku iliamriwa waondoke kwa sababu ya tank kubwa la petrol, ukaribu na nyumba na kelele za generator. Sijui kama waliondoka!
Mpige mkwala mama yako, wewe umeshakuwa mkubwa na umesoma. Asifanye maamuzi bila kukushirikisha. Next atakuambia kauza hapo anapoishi!
Tatizo elimu, mama yangu darasa la saba enzi za mwalimu ngoja nitamuuliza kama hata mkataba wa mauziano anao.
lakini walikosekana baadhi ya ndugu kujaribu kutoa msaada wakati wa makubaliano?
mimi naona anaweza kwenda mahakaman na kudai haki yake na kuraise objection that aliingia kwenye mkataba kwa kudanganywa(fraud) coz wao c walmwambia hawajeng mnara lakn matokeo yake wamejenga