Naomba msaada wa mawazo/mkopo/udhamini au ushirikiano kwenye biashara hii iliyopo ili ipanuke

Naomba msaada wa mawazo/mkopo/udhamini au ushirikiano kwenye biashara hii iliyopo ili ipanuke

Joined
Oct 24, 2019
Posts
34
Reaction score
32
Utangulizi.
Kutoka kwa mwanafunzi na mjasiliamali mimi ni mwanafunzi katika ngazi ya elimu ya juu mwaka wa pili hapa dar,nikichukua shahada ya teknolojia habari na mawasiliano{ICT} mwaka jana nilipitia changamoto za kimaisha hali iliyonipelekea kusitisha masomo yangu kwa muda hivo sikua na budi ya kutafuta namna nyingine ya kuishi kwa kujiiingiza kwenye biashara ndogondogo ambapo nilianza kununua mchele na unga soko langu kubwa likiwa majirani marafiki na wanachuo pia eneo la biashara hiyo ilikua nyumbani ninapoishi kwa sasa.

Kwa jitihada na mipango niliyokua nayo biashara hiyo ilinisaidia kunipa mahitaji yangu ya muhimu pia nilipata kutunza pesa hatimae nikachukua frem kwa ajili ya biashara hiyo nimeweza kutanua biashara yangu na kupata kutokana na kukua kwa soko mahali nilipo wakati najaribu kukuza biashara ila changamoto ya mtaji. Lengo, nikiwa mjasiliamali nimefanikiwa kupanga frem ya biashara eneo mabibo Dar nauza duka la kawaida na mtaji wake ukiwa na tathmini ya laki tano gharama ya vitu nilivyonavyo ukiachilia mbali capital assets.

Kiu yangu nikufanikiwa katika nyanja ya biashara ila mtaji unakua kikwazo kwa kua natamani biashara ikue kutokana na soko nililo nalo hadi sasa ila nashindwa kutokana na hali yangu ya kiuchumi.

Ombi langu, naomba msaada wa mawazo/mkopo/udhamini au ushirikiano kwenye biashara hii iliyopo ili ipanuke na kua kubwa naamini katika biashara pia nina uzoefu kwenye biashara hivo natamani sana biashara inayokua,pia hata kwa kuunganisha nguvu kwenye biashara kwa faida za pande zote mbili pia natamani kama itatokea Mahali pa biashara, nipo mabibo mwisho yeyote atakaetokea kuunganisha nguvu au kunipa msaada wa namna yeyote ile . Hivo basi kwa unyenyekevu naombeni msaada ili niweze kupanua biashara yangu nipo tayali kwa msaada muda wowote kuanzia sasa.
Wenu mipangoMikubwa.

Kwa mawasiliano +255 787357219
 
Back
Top Bottom