Naomba msaada wa mawazo wajenzi nataka kuhamia kwenye nyumba yangu

isley

Member
Joined
Sep 24, 2016
Posts
48
Reaction score
83
Nataka kuhamia kwangu mwaka huu nimepiga nyumba plasta Bado kuweka vifaa vya umeme awamu ya pili, Bado draft na vingine vingi.. je nikitafuta hela ya madirisha yanaweza kuwekwa bila kufanya skimming ili nihamie mengine nitaendelea nayo taratibu? Na je kabla ya kuweka madirisha ya aluminium ni lazima nipige rangi nyeusi kwenye madirisha?

Shimo la choo Bado ila chemba zote tayari, napata utata wa mashimo wengine wanasema nichimbe mawili wengine moja Sina uzoefu hapo Bado namtafuta mawazo
 
Hongera kwa hatua hiyo.

Ngoja waje kukupa muongozo
 
Fanya skimming kwenye madirisha peke yake. Paka rangi kwenye grill kabla hujaweka aluminium ili kuepusha kuchagua vioo baadae ingawa sio lazima sana
Upande wa shimo anza na shimo dogo kwanza. Kama huna familia kubwa utadumu nalo kwa muda mrefu sana. Hela ya kuchimba shimo kubwa unaweza kuitumia kuanza kutengeneza draft kwanza
 
Asante Sana sikujua kama inaweza kufanya skimming kwenye madirisha peke yake kwanza Asante kwa ushauri
 
Inategemea na uwezo wa kifedha (mfuko) wako kwa sasa na kodi yako inaisha lini. Kama mfuko hautoshi na kodi inaisha miezi miwili ijayo fanya yafuatayo
1. Malizia shimo la choo moja
2. Fanya finishing ya choo kimoja public toilet weka tiles na mfumo mzima wa maji taka katika choo hicho pia weka na dari
3. weka makaratasi madirishani, mlango wambele na wa nyuma weka signboard pia mlango wa public toilet weka alminium window
4. fanya wiring sitting room na vyumba viwili tu ili uweze kupokelea umeme. kama umeme upo mbali waone mobisoli watakukopesha solar yenye nguvu kwa bei nafuu na utakua unalipa kidogo kidogo kila mwezi
5. Baada ya hapo hamia changamoto utakazoanza kukutana nazo ukiwa ndani utaanza kuzitatua moja baada ya nyingine na utajisikia amani sana ukiwa kwako

NB
Kipindi cha finishing ni kigumu sana na kina gharama sana. angalizo usije pata vidonda vya tumbo maana kila ukipata pesa utakua unawaza nyumba tu mpaka kuvaa nguo mpya utaona ni anasa sana
 
Hongera na ngoja waje kukupa muongozo...
 
Ha ha ha ha kweli unaweza pata vidonda, Asante kwa mawazo mkuu na kwa muda wako
 
Fanya skimming kwenye madirisha peke yake. Paka rangi kwenye grill kabla hujaweka aluminium ili kuepusha kuchagua vioo baadae ingawa sio lazima sana
Upande wa shimo anza na shimo dogo kwanza. Kama huna familia kubwa utadumu nalo kwa muda mrefu sana. Hela ya kuchimba shimo kubwa unaweza kuitumia kuanza kutengeneza draft kwanza
Draft ndio nn?
 
Nicheki mkuu naweza kusaidia mwongozo katika haya mambo yaujenzi 0755918095 nitakupa ushauri bule naweza kufika sait bila malipo kama sio mbali mengi kwenye nyumba nafaham na ninafanya kasoro umeme namaji
 
hamia mtaalam mrad umefanya wiring set up yot ya umem na maj draft ingependeza kupiga kabla ya plasta kuzuia michaniko ila sio mbaya
maliza public toilet kwa ukamilif wake hio ndiobofis muhim .vymbq vingine utamaliza taratib humohumo
rang piga kabisa utachqfua kioo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom