Heshima kwenu wakuu. Nina mdogo wangu wa kike amemaliza form four mwaka jana. Amepata four ya 31. Ana D ya chem, bios, maths na kiswahili. Yaliyobaki ana F. Nilipo hapa nawaza asome chuo gani? Nimeangalia nursing wanasema lazima awe na physics na ye aliacha form two. Naomba msaada, kuna chuo cha mambo ya kilimo anachoweza kusoma? Na vyuo vingine ambavyo anaweza kupata nafasi kwa ufaulu wake.
unajua kuna kozi mtu unasoma aafu unarudi mtaani hakuna cha kufanya. Mfano public administration utamtawala nani? Ndo maana nikafikiria hata kilimo asipopata ajira anaweza kuanza ufugaji au kulima mashamba. Kufeli kusiwe kigezo cha kumpeleka mtu hata vyuo ambavyo ni vya kisanii mkuu.!