Mkuu hongera kwa kutaka kujikwamua na umasikini
- Ila naomba uelewe vifuatavyo
1. Kikundi na SACCOS ni vitu viwil tofauti kabisa
2. Uanzishwaji wa SCOS ina idadi ya members na kikundi kina idadi ya members
3. Na SACCOS mara nyingi inadili na kuweka na kukopa na sijajua kama ndo lengo lenu la kuweka na kukopa
4. Kikundi ndo kinaweza fanya mambo mengi hata likiwemo la kuweka na kukopa
5. Mkianzisha kikundi kuna furusa za kibiashara mnaweza kuzikosa kwa sababu kikundi kufanya biashara na makampuni inakuwa ngumu kidogo na mtakuwa mnabanwa na sheria za vikundi na mambo ya TRA
6. kama mko siriaisi na kama mmeisha jipanga na tiyali mna mawzo yenu ya biashara mnaweza tu fungua kampuni ya mtaji mdogo na hata mkienda TRA kitengo cha Elimu kwa walipa kodi watawapa elimu ya Ulipaji kodi ya makampuni mtaona kwamba ni rahisi sana kuliko kuogopa kampuni kisa TRA,
7. Kwa dunia tuliyopo sasa kampuni inaply sehemu kubwa sana katika kufanya biashara yoyote ile na si kwamba kampuni kuindesha ni mpaka muwe na mtaji wa mamilioni, no kuna kapnu zinasajiriwa kisheria na zinamitaji ya elfu 80, tu