Naomba msaada wa tafsri ya haya maandishi

umeyapata wapi? ulienda kwa mganga wa kutumia kitabu akakupa au umekuta tu kwako hujui ilipotoka ?
Tuanzie hapa kwanza
Nimeyakuta nyumbani kwangu yani chumba ninacholala, kwenye maeneo tofauti ndani ya Chumba
 
Habari wakuu,

Naomba kupewa tafsiri ya haya maandishi hapa chini
Kwa kipande cha kwanza chenye visanduku vye namba 100, 1, 7, 200 na kuendelea kuna maneno haya "كُلَّمَا دَخَلَ عَلَیۡهَا زَكَرِیَّا ٱلۡمِحۡرَابَ وَجَدَ عِندَهَا رِزۡقࣰاۖ قَالَ یَـٰمَرۡیَمُ أَنَّىٰ لَكِ هَـٰذَاۖ قَالَتۡ هُوَ مِنۡ عِندِ ٱللَّهِۖ إِنَّ ٱللَّهَ یَرۡزُقُ مَن یَشَاۤءُ بِغَیۡرِ حِسَابٍ" Kwa maana ya "Whenever entered upon her Zakariya [the] prayer chamber he found with her provision. He said, "O Maryam! From where for you (is) this?" She said, "This (is) from Allah. Indeed, Allah gives provision (to) whom He wills without measure."

Hicho ningine nimeshindwa kuona vizuri.
 
Nimeyakuta nyumbani kwangu yani chumba ninacholala, kwenye maeneo tofauti ndani ya Chumba
Sawa ndugu, Hiyo inaitwa talasim wako wanaosema kuna talasim nzuri na mbaya ila zaidi ya 90% huwa ni mbaya tu na hutumiwa na washirikina wa kiganga kufarakanisha watu, kuwasukumia majini na mikosi na mambo yenye kufanana na hayo.
Sasa hiyo ya kwako sijui inahusiana na nini ila nakushauri japo sijui wewe ni dini gani ila mtafute sheikh ambaye kasimama kwenye misingi sahihi ya dini jaribu kuuliza katika maeneo yako nakwambia hivyo kwa sababu unaweza mfata sheikh kumbe ni sheikh shehena nayeye ndio walewale washirikiana ukimpta muonyeshe kisha atakusaidia jinsi ya kuvunja nguvu za hiyo talasim.
kama wewe ni muislamu soma surat ikhilasw, falaq na nass zote mara tatu au saba kisha pulilizia hewa kwenye maji yaliyo ndani ya ndoo kisha tumbukiza hizo talasim acha huko ndani ya siku nzima kisha nenda kamwage maji na hayo makatasi.
una swali zaidi au unahitaji ufafanuzi zaidi? feel free to ask.
 
Nimekuelewa vizuri sana
 
Asante sana, Kuna hii nyingine nimeikuta tena zikiwa kwenye bahasha kwa pamoja, naomba msaada, nimechoka sana, ndoa yangu haina amani. Ni kununa na magomvi yasiyo na sabau
 

Attachments

  • IMG_20240918_064312_868.jpg
    636.9 KB · Views: 2
Njia nzuri ya kuteketeza ni ipi?
Kuchoma moto na kufukia majivu,
Nasema hivi kwa sababu katika ushirikina wengine wanachanganya na aya za quran au hadithi za mtume kwa mfano kwenye hiyo karatasi yako moja nimeona kitu kinafanana na hapa nilipobold

Surah_Al-Im'ran_: Ayah 37

فَتَقَبَّلَهَا رَبُّهَا بِقَبُولٍ حَسَنٖ وَأَنۢبَتَهَا نَبَاتًا حَسَنٗا وَكَفَّلَهَا زَكَرِيَّاۖ كُلَّمَا دَخَلَ عَلَيۡهَا زَكَرِيَّا ٱلۡمِحۡرَابَ وَجَدَ عِندَهَا رِزۡقٗاۖ قَالَ يَٰمَرۡيَمُ أَنَّىٰ لَكِ هَٰذَاۖ قَالَتۡ هُوَ مِنۡ عِندِ ٱللَّهِۖ إِنَّ ٱللَّهَ يَرۡزُقُ مَن يَشَآءُ بِغَيۡرِ حِسَابٍ
Tena Mola wake Mlezi akampokea kwa mapokeo mema na akamkuza makuzo mema, na akamfanya Zakariya awe mlezi wake. Kila mara Zakariya alipo ingia chumbani kwake alimkuta na vyakula. Basi alimwambia: Ewe Maryamu! Unavipata wapi hivi? Naye akasema: Hivi vinatoka kwa Mwenyezi Mungu; na Mwenyezi Mungu humruzuku amtakaye bila ya hisabu.

Haya sasa jiulize maandishi haya yana uhusiano gani na hayo madude mengine yaliyowekwa pamoja kwenye karatasi zako? Ndiyo maana nikakushauri ni bora uchome moto tu.
 
Asante sana
 
Jambo usilolijua lisikusumbue.
Choma Moto,naamini Mungu kuwa uko salama,songa mbele na Mambo yako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…