Naomba msaada wakuu

Naomba msaada wakuu

dos.2020

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2009
Posts
11,880
Reaction score
10,372
Labda nianze nyuma kidogo. Mimi ni mwanamme, Miaka zaidi 10 nyuma nilipatwa na tatizo lilonisumbua sana. Lilianza hivi, Nilikua Napata maumivu wakati wa kukojoa, mambo yakaendelea mwisho nikawa nakojoa mkojo unaochanganyika na damu, Yakazidi kuendelea mwisho nikawa natoka usaha. Sihivo tu yaliambatana na homa kali kwa mda wote wa siku, Kuanzia eneo la kitovu mpaka kwenye magoti mulikua munawaka moto mithili ya kuchemka kabisa. Namwisho ikawa nashindwa kuzuia mkojo, Mkojo ukija nashindwa kuuzuia unatoka tu na tena wenye maumivu, Na ilkua haizidi dakika 15 nakojoa tena. Yalidumu kawa takriban miezi 6 na miezi mitatu ya mwisho hali ilikua mbaya kabisa. Yote haya yananitokea nilihangaika maspitali mpaka nimekata tama kabisa achilia tiba walishindwa hata kujua tatizo ni nini hasa. Nikaachana na Spitali nikaanzia kubwia madawa yakienyeji mpaka nikapowa. Na binafsi sikujua hasa ni dawa gani ilioniponesha mana nilikua nabwia tu ninachopata.

Tatizo lilihama lakini ndani ya miaka 10 limenirejea tena mara 3, Ila nilichogundua wakati yaliporejea ni kuwa nikinywa maji mengi sana yani kuanzia lita 5 kwa siku ndio afadhali ninapopata. Kwaiyo kila yaliporudi nilikua nakunywa maji mengi sana kwa siku na mwisho ndani ya mwezi tatizo linapote.

Nashukuru sasa nina karibu mwaka wa 4 halijarudi.

Sasa nakuja kwenye kesi yenyewe. Mana nimeona nilieleze nahilo pengine linaweza au nahisi linaweza kuwa namahusiano. mazingira yangu yakikawaida yapo hivi, Inanilazimu kwa siku ninywe maji yasipungue lita 3 kwa kipindi kama hiki cha joto na yasipungue lita 2 kwa kipindi cha baridi. Chini ya hapo lazima nitapata tabu kwenye kukojoa, Nitakua nahisi maumivu, michonoto, na mkojo wenye warangi kali. Hapo mbali nasiku ninazokula vyakula kama maharage, Supu, Muhogo na mboga yake inanilazimu niageze dozi bila ya hivo hali ndio kama hivo. Na mda mwengine huhisi kama viungo vangu vya uzazi vinachemka kabisa kwa ujoto kabla na baada ya haja. Nimekua nikiishi nalo kwa mda mrefu Ila nilichogundua Watu wengine hawapo kabisa kama mimi, Mtu anaweza kunywa hata glass moja tu au mbili za maji kwa siku na akapata haja ndogo bila kupata tatizo lolote kwanini iwe hivi kwangu mie? Sio kama sipendi kunywa maji Napenda sana kunywa maji mengi mana nafahamu ya faida nyingi za kiafya Lakini kwanini lazima mpaka iwe hivo kwa mie tu? Bila yashaka nitakuwa na matatizo, hofu yangu yasije kuwa makubwa huko mbeleni.

Sasa nataka kuyafahamu matatizo yangu na nijue nianzie wapi kuyatatua mana umri unakwenda na uzee unakaribia na huko uzeeni ndio matatizo mengi huvumbuka.



Naombeni msaada, Ushauri, Vyakula vya kutumia, Dawa, na mengine ili niweze kujisaidia wakuu.

Nisadieni wakuu akina MziziMkavu na wadau wengine.
 
sielewi sana unaposema umetembea hospitali nyingi bila mafanikio, sijui ni hospitali za wapi hizo.
Mkuu mbona vipimo vipo, wataalamu wapo, wewe uko wapi huko.

Kwanza pole sana.
Halafu kama uko kanda ya ziwa jipitishe bugando pale, na kama uko ukanda wa mashariki basi tembelea Muhimbili, kama kanda ya kati fika Benjamini Mpaka Dodoma.
Si rahisi kusema eti tatizo halikujulikana wakati vipimo vipo tena vingi.
Daktari mmoja akikuambia tatizo halionekani, hama hapo tafuta msaada kwingine, wakati mwingine kuna madaktari wapo kwenye facilities ambazo haziwawezeshi kujua au kugundua vitu vingi, si makosa yao.
 
Back
Top Bottom