Naomba msaada wenu kuhusu usajili wa chuo

bekadula

Member
Joined
Oct 11, 2014
Posts
38
Reaction score
0
Jamani nisaidieni kidogo ushauri nimechaguliwa UDSM education nikataka kufanya transfer TCU kwenda NIT lakini nafasi wakasema zimejaa nikaenda mpaka NIT nikakutana na mhadhiri ambae tunafahamiana nikamueleza shida Yangu akanipeleka ofisi ya msajili akasma nafasi bado zipo yule msajili akaniandikia barua kwamba wamenikubalia kujiunga hiyo barua kawaandikia TCU na akanambia nikatoe copy ile barua original niipeleke TCU na ile copy niiache pale NIT nikafanya kama alivyonielekeza.

Nilipofika TCU mapokezi nilipompa ile barua akanaiambia nikalipie benki 30000 halafu niambatanishe risiti na ile barua nikaenda benki na nilivyompa akazibana kwa pamoja apanda nazo juu. Saa juzi TCU wametoa tangazo kwenye website yao kwamba kuna watu wameenda kujisajili chuo moja kwa moja hivyo TCU hawatowatambua sasa na Mimi nna wasiwasi niendelee kuwasubiri TCU au nikafanye registration UDSM ? Nawaombeni msaada wenu wa mawazo
Niatafurahi sana kama nitapata mawazo ya watu wengi
NAWASILISHA
 
wasubiri tu, kwasababu wameshaiona barua yako. na huko ud usiende kujisajili kwasababu majina yakitoka umepangwa nit utasumbuka bure
 
Hilo swala linaweza kukusumbua pia kwenye kupewa mkopo kuwa mfatiliaji
 
Nenda TCU kwa huyo dada wa mapokezi umuulize anaweza kukupa mwanga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…