Tumsifu Samwel
JF-Expert Member
- Jul 30, 2007
- 1,407
- 161
Hapa ina maana unataka kufungua Internet Cafe ya nyumbani ambayo kila mmoja anahitaji Computer yake iunganishwe na mtandao.Heshima kwenu wanaJF
nina connection ya internet ambayo ni wired nahitaji kuibadilisha kuwa wireless.nimefikia uamuzi huu kwani hapa nyumbani kwangu nina vijana wangu ambao kutwa nzima wana shinda wa kitumia internet,hivyo kitendo hicho kina wanyima wengine kutumia mtandao,hivyo nimeonelea ili kuondoa mzozo huo nifanye utaratibu wa kuingeuza kuwa wireless ili kila mtu awezekutumia akiwa chumbani kwake badala ya kutengemea Computer moja ambayo imeonganishwa na mtandao. Naomba ushauri wenu nitumie njia gani kuibadilisha kuwa wireless,je ni vifaa gani ambavyo na paswa kuvinunua ili kuweza kufanikisha kusudio langu?
......Nadhani kuna maalum cha kuunganishia computer zaidi ya moja. Ukipata hicho nadhani utakuwa umepunguza usumbufu....
vijana wangu kila mmoja ana laptop yake,hivyo kama kutakuwa na wireless kila mmoja atapata fursa ya kutumia mtandao bila kumpa mwenzake usumbufu. Speed ya connection yangu ni 1mbps ambayo itawatosha sana endapo watakuwa wanatumia wote kwa wakati mmojaHapa ina maana unataka kufungua Internet Cafe ya nyumbani ambayo kila mmoja anahitaji Computer yake iunganishwe na mtandao.
Nadhani kuna maalum cha kuunganishia computer zaidi ya moja. Ukipata hicho nadhani utakuwa umepunguza usumbufu.
Wataalam wa haya masuala waendelee kuchangia na kutoa msaada zaidi.
Idimi asante sana kwa ufafanuzi wako mzuri.Naitaji kutumia wireless kwani computer zote zina wireless card.Ni kweli, na kifaa hicho kinaitwa 'wireless router' au 'hub'. Router zipo za aina nyingi sana kulingana na mahitaji yako, lakini kwa Dar nyingi zilizo sokoni ni D-Link, Huawei, Panasonic na Sony.
Ufanyaji kazi wa router au hub ni kwamba, ule waya wa mtandao ambao kwa sasa umeuweka katika kompyuta yako, unaingiza katika inlet ya router, then router ina matoleo kadhaa (iwapo ni ya waya) kwa ajili ya kuchomekea nyaya za kutumia mtandao katika kompyuta nyingine.
Kwa wireless router, kawaida inakuwa na aerial ambayo husambaza mtandao ktk maeneo ya karibu kwa njia ya aerial. Kwa kawaida kunakuwa na software maalum (yenye password) ya kudhibiti uingiaji holela ktk mtandao husika pamoja na firewall.
Ukifika katika duka lolote ambalo vinauzwa vifaa hivi watakupa maelezo na msaada zaidi, wa namna ya kutumia kifaa hiki.
kila la kheri
Ubarikiwe sana Idimin,
Yo Yo asante sana mkuu.Ushauri zaidi tafadhali kwa mdau yoyote mwenye idea na haya maswala.mkuu angalia
YouTube - Broadcast Yourself.
YouTube - Broadcast Yourself.
YouTube - Broadcast Yourself.
zipo video nyingi youtube...unaweza kuziangalia na kufanya mwenyewe ni rahisi sana....