Naomba msaada wenu wakuu nasumbuliwa na sulphur allergies

kabango

New Member
Joined
Oct 25, 2015
Posts
4
Reaction score
5
Naomba msaada wenu wakuu mimi nina sulphur allergies nafanyaje niweze kuondokana na ili tatizo kabisa mana product nyingi madukani zina sulphate najikuta nameza dawa mara kwa mara nisaidieni hata kama kuna dawa za kienyejiza kumaliza tatizo kabisa
 
Hiyo allergy ipoje mkuu ? Jaribu kuielezea vizuri ili hadi sisi hkl tuijue huenda ukasaidiwa
Natokwa na vipele vingi vikiambatana muwasho mkali...endapo nitatumia product yenye mchanganyiko wa madini ya sulphate kwenye ingredients lkn hata nikila kuku broiler mayai tunayo ita ya kizungu nateseka na hii allergy jamani maji ninywe Kilimanjaro tuu hayana sulphate lkn vitu vingi vina iyo
 
ooh, pole mkuu ngoja wataalamu waje utasaidiwa tu.
 
hiyo allergy sasa itakuwa imeambatana na hofu yako..
Mimi pia nina allergy na sulphur, nimegundua hilo miaka mingi iliyopita enzi hizo ALU hazipo nilikunywa SP ikanionesha kazi.
Lakini maji ya kila kampuni nakunywa, mayai ya kisasa niliwa wala hayaniletei shida, attention yangu imebaki kwa madawa ya hispitali tu ndio huwa nakuwa makini ambapo napo bado yapo mengi sana yasiyo na sulphur.
Wewe ondoa hiyo hofu, usifikirie sana juu hata ya maji, usihisi kama yatakudhuru, ingekuwa hivyo basi hata dawa za meno zingekudhuru
 
Dawa ya meno ninayo tumia ni Colgate Sensitive PRO-Relief iyo haina kabisa sulphate...chochote chenye sulphate kwangu ni tatizo. Unaponiambia niambia maji naweza kunya yoyote niondoe hofu sikuelewi. Wakati kwenye Ingredient imeandikwa kuna sulphate 9.5 sasa hapo inaniachaje kwa mfano
 
Jitahidi sana kula matunda yenye elements za antioxidants...... Kama strawberry, papai, lemon, embe, na kadhalika,

Kunywa sana juice organic achana na za viwandani.....


Achana na soda na bia na beverages za kiwandani zote yaani ikitokea iwe ni bahati mbaya sana....umekosa cha kunywa ndio unatumia....

Kiasi cha Acid kikishuka mwilini mwako sulphur itakuwa balanced na itatumika kufanya kazi zake za msingi na sio kama sasa ambapo imezidi sasa inakupa shida mwilini badala ya kuwa ni ahuweni......
 
Kama mm vile same problem
 
Na ndio hiyo hofu ninayoisema unakuwa mbishi.
Hivi unajua watu wengi wenye allergic reactions mpaka ukubwani huwa wanakuwa ni matokeo ya kuzembea katika vitu fulani fulani hasa utotoni?!?
Hivi unajua sulphur iko kwenye vyakula vingi? unakula nyama, dagaa, maziwa, vitunguu vyote hivi na vingine vingi vina sulphur, je huwa vinakudhuru? vile unaogopa maji kweli yatakudhuru maana mwili na akili vyote vinahisi si salama.
Hicho kiwango kilicho kwenye maji ni kidogo sana mkuu. Sulphur ikiwa nyingi kwenye maji namna ya kutambua ni harufu, maji yanakuwa na harufu mbaya ya gesi ya hydrogen sulphide, na hii inatokea sana kwa maji ya kisima, si ya kiwandani.
Kinginr chenye sulphur nyingi ni madawa, maana inakuwepo purposely.

Kwa msaada zaidi ingia google jifunze kuhusu sulphur(salfa) na sulphite(sulfite) allergies, ni vitu viwili tofauti ila huwa vinaonekana kama sawa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…