kindboy
Senior Member
- Dec 11, 2010
- 142
- 28
Habar5i za asubuhi wanajf,Nimekuwa na plansza mda mrefu za kutaka kuingia kwenye ujasiliamali katika kilimo , baada ya maandalizi yangu kwa mda sasa nimefikia wakati nataka kutimiza ndoto zangu za kuingia katika hii biashara ya kilimo,kulingana na reaserch yangu ndogo nimeamua kujikita katika kilimo cha umwagiliaji na hasa katika mazao tajwa hapo juu yaan, matiki maji,nyanya, vitunguu na hata pilipili hohoo.kwa maana hiyo basi nimejaribu kufutilia maeneo ambayo yanaupatikanaji wa maji kwa urahis na chanzo cha uhakika nikambiwa Hedaru kuna eneo ambalo liko karibu na na mto pangani na mashamba yanapatikana , kwa kukodi na pia kununua, mpaka sasa sijajua ni eneo lipi hasa hapo Hedaru ama kijiji kipi? ambacho naweza pata hilo eneo . nilikuwa naomba msaada kwa wanajf wenzangu ambao wanalifahamu eneo hilo wanijulishe nakunipa mwanga wa namna ya upatikanji wa hayo mashamb nilikuwa nahitaji kuanza na kama Acre 4 mpaka 5 hivi kwanza kulingana na upatikanaji wake na bei zake pia.Aukama kutakuwa na maeneo kama hayo jiran na eneo hilo na yenye sifa kama hizo ningeomba nifahamishwe pia plse ,.natanguliza shukurani zangu kwenu na pia nategemea kupata ushiriano kwa wataalam wa biashara ya kilimo na masoko yake pia