Naomba Muongozo wakuu; nataka kuanza biashara ya silaha za jadi zilizoboreshwa

Mangi flani hivi

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2016
Posts
2,026
Reaction score
3,107
Wasalamu,

Wakuu maisha yamebana sana na kila mtu anatakiwa kujiongeza ili mambo yaende. Mimi nina kautalaam kidogo ka silaha za jadi ie: upinde, mishale, mikuki na kadhalika.

Nilipata kuletewa zawadi ya upinde wa kisasa ambao ni tofauti kidogo na hizi za kwetu. Umeboreshwa na unampa mtumiaji uwezo mkubwa wa kutumia kwa ufanisi mkubwa.

Sasa:
Nimepata wazo kwa sababu za kiusalama, na kwasababu ni biashara ambayo inafanyika hata kwenye masoko yetu ya mitaani na kwa sababu bado ni silaha ya jadi, nimeona niagize za kutosha ili niuzie na wenzangu. Wasiwasi ni kuwa zama hizi sio zile.

Ushauri wakuu, nianzeje, na je nitaeleweka?
 
Ukitengeneza za hivi ntakuwa mteja wako.
Iwe na trigger
Huwa nataka ninunue nje ila sijui kama ntaruhusiwa kuingiza nchini.
Itakuwa unazijua hizi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…