Franco Zetta
JF-Expert Member
- Nov 3, 2014
- 1,661
- 843
Wadau na Wabobezi wa Historia ya mapambano ya Ukoloni katika Tanganyika kuna hawa Mashujaa Wawili Waafrika ambao kwa namna tofauti na Wapigania Uhuru wengine wao wali sababisha usumbufu mkubwa kwa wakoloni na walowezi katika miaka ya 50 na hasa katika Mkoa Watanga na mapango ya Amboni yakawa maficho yao,Osale Otanga akijulikana kuwa na uraia wa Kenya na Paulo Hamisi akisemwa alikuwa Mzalendo mwenye asili ya Mtae(Lushoto) tafadhari mwenye kuielewa historia yao na mapambano yao atujuze.