Naomba mwenye link ya matokeo ya kachaguliwa kidato cha kwanza mwaka 2024 atume

Sasa subiri nakuwekea matokeo ya mtoto aliyepata wastan wa A zikiwepo hesabu na sayansi na bado akapangwa shule za kata mwaka huu,ndugu usikatae haya mambo yametukuta na watu wanalia hapa.
 
Mtoto wangu ana B ya uraia tu lakini kapangiwa day..
 
Mtoto wangu ana B ya uraia tu lakini kapangiwa day..
Sawa sio tatizo,ishu inakuja kwanin sio wote hawa ambao nao wana wastani wa B alafu wamepangiwa shule za bweni ikoje hii??
 
Mbna zote nzuri tyuuh
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Alafu ishu ya eti shule zipo 38 sio kweli mzee,
Jaribu kufuatilia upya,kumbuka kila mwaka kuna shule mpya zinaanzishwa nyingi sana,ndani ya miaka ya samia zipo shule za bweni kwa ajili ya kudato cha kwanza zaidi ya tano zimeshaanzishwa,shule unazosema wewe labda kipindi tunasoma sisi miaka ya 1990s
 
Mkuu unaweza kuwa sahihi,kuna ushubwada mwingi sana kwenye elimu yetu..
 
Hizi zote ni public schools of Tanzania
Moshi ufund,old mosh,lyamungo,kifaru,kilakala,msalato,tanga ufund,bwiru,minaki,pugu,kibaha,ilboru,mzumbe,kisarika,kisimiri,jokate mwegelo mlingano,kantalamba,azania,jangwani,toangoma,ashira girl,weruweru,balangdalau,tumaini.

Kuna shule mpya zaidi ya kumi ndiomana kila mwaka wanaokua selected wanaongezeka kiidadi,hizo ni chache ninazozifahamu,zipo nyingi sana za o level.

Alafu kama wewe unao uwezo wa kuwapeleka wanao private ni wewe brother unafikiri kwanini zipo hizi shule kama ilboru,kibaha,moshi ufundi,ifunda kilakala,korogwe,kama ungejua usingeweza kuongea hivi eti watawapeleka watoto wao private nzuri tu.
Usilete stori za yohana mjinga hapa aliyetumwa na mama yake kwa msisitizo akanunue mafuta ya kupikia huku akiambiwa hakikisha unaweka hela mfukoni ili isipotee,yohana akakariri kwamba ili mafuta yasipotee ngoja niyamimine mfukoni nicheze mpira nikifika nyumbani nayatoa nampa mama apike.
 
Hakuna cha rushwa wala nini hebu acheni ujinga ninyi mtoto wa dada yangu kapata wastani wa B ila kachaguliwa shule ya ufundi na hatukutoa rushwa
 
Leo hii kafanyiwa mwanangu dah,mwanangu kapiga A za hesabu,sayansi,kiswahili na kingereza zingine B cha ajabu kapangwa shule ya kutwa.kwani wanatumia vigezo gani?naomba mnisaidie kujua.
Unataka tukose hata wa kuchangamsha darasa mkuu!?
Usihofu huku mwakani tumepanga kufanya makubwa dogo atafika mbali
 
 
Hakuna cha rushwa wala nini hebu acheni ujinga ninyi mtoto wa dada yangu kapata wastani wa B ila kachaguliwa shule ya ufundi na hatukutoa rushwa
Ipo namna ndugu,wewe usiseme eti hakuna cha rushwa,sawa hatujakataa kwamba hakuna rushwa ila tungefafanuliwa wanatumia vigezo gani kuwapanga hawa watoto kwenda kidato cha kwanza?mimi ninao watoto mapacha wamemaliza msingi hizi za serikali,mmoja amepiga wastani wa A na Hesabu ana A bado kapangwa day school,doto amepiga wastani wa B nae kapangwa day school sasa sijui naomba nifafanulie nielewe ndugu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…