Jamaa yenu hapa ninayo shauku kubwa ya kujifunza kutengeneza magari pamoja na pikipiki kwani maisha niliyo nayo mara baada ya kutoka chuo hayasomeki hivo nimeona ni vema zaidi nikapata japo ufundi stadi ambao utaniwezesha kupata riziki ya kuishi wakuu.
Lengo langu ni kupata materials au source zozote zitakazoniwezesha kujifunza ufundi huo theoretically kwanza halafu baadae ndo nakuwa nasogea gereji napractice polepole mpaka kitakapoeleweka. Mwenye kuweza kunisaidia kwa hilo anakaribishwa sana wakuu
Kutengeneza magari kwa ujumla wake itakuwa ni ndoto.
Gari ina mifumo mingi.
Kuwa specific unataka ubobee kwenye ujuzi wa mfumo upi wa gari:-
- Umeme
- Engine
etl
Sehemu sahihi ya kuanzia ni VETA au DIT au NIT, ila sio kwa huo utaratibu wa kuanza na theory, mafanikio itakuwa ni kidogo au hakuna kabisa, Ujuzi husika ni too practical, na sio kinadharia, Kumbuka wahitimu wa vyuo vikuu wanafundishwa kushika spana na mafundi/ vijana wenye ujuzi wengi wao hata chuo hawajafika.
Iwapo hauko tayari kwenda vyuo rasmi kupata huo ujuzi basi fanya tafiti na upate gereji kubwa inayojishughurisha na magari / piki piki, Ongea na wamiliki na watakupa utaratibu wao wa wewe kuanza kujifunza, Gereji hakuna maswala ya notice za kusima.
Piga uwa ni lazima uwende kwanza gereji ama chuo cha ufundi,kwenye ufundi kusoma vitabu bila vitendo(practical) jnatwanga maji kwenye kinu.
Afadhali uanze kwanza gereji au chuo kisha uanze kutafuta vitabu taratiibu kulingana na jinsi unajifunza.
Tafuta geregi ya ufundi wa magari "MVM" kwa kuanzia Kisha fanya prack kwa miezi kazaa"Baada ya hapo utakuwa uko tayari kupiga short course ya Motor Vehicle Mechanic,M.V.M.