Sasa ndio wananchi muelewe wazi kabisa ni Chama cha namna gani kilichopo madarakani na umuhimu wa kukiondoa madarakani kwa kura zenu. CCM haiko pale Ikulu kwa manufaa ya mwanachi wa kawaida, iko pale kwa manufaa ya kikundi kidogo kilicho hodhi madaraka na sasa kinajaribu hata kuhodhi mustakabali wa nchi yetu.
Na ukijua nani yuko behind CCM ndugu yangu utalia machozi.
Ni hivi. Usitegemee CCM itakubali mabadiliko ya kweli ya Katiba ya nchi. Siku CCM inakubali mabadiliko ya katiba au Katiba mpya huo ndio mwisho wa CCM. Sasa kama wako madarakani unafikiri watakubali hayo yatokee ndugu yangu! TUMIA AKILI YAKO. Na JK sio mjinga kiasi hicho. Hawezi kukubali CCM ifie mikononi mwake. Yeye sio Gorbachev wa Tanzania.
Elewe pia kuwa CCM inawafuasu wengi sana katika watumishi, wafanya biashara, na kadhalika ambao kwao si rahisi kuunga mkono mchakato ambao utapelekea CCM ikatoka madarakani. They have a lot to lose. Na kwa ufahamisho, ndugu yangu, kwa Watanzania wa leo, wa sasa, kinachothaminiwa ni maslahi binafsi. Taifa baadaye. Ni jambo la kusikitisha, lakini ukweli ndio huo.
Mtu yeyote mwenye akili timamu, mwenye kuthamini demokrasia ya kweli hangethubutu kutunga wala kuwasilisha kama muswada hiyo sheria ya mabadiliko ya Katiba ya nchi yetu kama ilivyotolewa. Lakini wako draftmen "watanzania" wametunga huo muswada na iko serikali ya "watanzania" wanaupeleke bungeni. NA KULE BUNGENI HUO MUSWADA UTAPITISHWA KUWA SHERIA kwa sababu wabunge wa CCM ndio wengi na wana maslahi kwa CCM kuendelea kutawala. Katiba ya sasa inawapendelea wao! Kwa kifupi KATIBA ISIYO YA WANANCHI ITAPITISHWA KWA MARA NYINGINE TENA. NA KWA SHERIA ILIVYO HUWEZI UKAPINGA MAHALI POPOTE. VYAMA VYOTE HAVIRUHUSIWI KUSHIRIKI KWA MAANA YA KUELIMISHA WANANCHI NA MAPENDEKEZO YATAPELEKWA KWA RAIS(M/Kiti wa CCM) PEKEE.
Mimi nasema kuwa hizi class struggles zitaendelea hata baada ya Katiba kuandikwa upya au kurekebishwa kwa matakwa ya CCM. Dunia imejaa mifano mingi sana ya mapambano ya wananchi dhidi ya serikali zao. Kinachoendelea mashariki ya kati ni mfano tosha. CCM ina sikio la kufa.
Katiba ya Wananchi itapatikana baadaye lakini sio hii na sio kwa mtindo huu. Kinachopelekwa bungeni ni sheria ya mchakato wa katiba ya CCM na JK.
MUNGU IBARIKI TANZANA.