Hapana, serikali ya mseto inaondoa demokrasia kabisa. Kama vyama vyote vitaunda serikali ya mseto then kutakuwa hakuna upinzani na tutakuwa tumerudia mfumo wa chama kimoja chenye matawi tofauti. Serikali ya kitaifa lakini siyo ya mseto. Kujenga kwa serikali ya kitaifa kunawezekana iwapo tutakuwa na utaratbu mzuri sana wa kutenganisha mambo ya serikali na mambo ya siasa. Yaani serikali na vyombo vyake visijihusihe moja kwa moja na kampeini zozote za kisiasa. Waziri asitumie nafasi ya uwaziri kupiga debe la kisiasa. Chini ya utaratibu huo, inawezekana chama chenye serikali kuhusisha baadhi ya wanachama wa vyama vya upinzani kwenye serikali yake kama ambavyo Marekani wanafanya. Waziri wa Ulinzi katika serikali ya Klintoni alikuwa ni Republican william Cohen, Waziri wa uasfirishaji katika serikali ya Bush alikuwa Norman Y. Mineta ambaye ni Democrat, na sasa serikali ya Obama ina William Gates ambaye ni Waziri wa Ulinzi akiwa ni Republican.