Naomba mwongozo wa kisheria

Singwa

Member
Joined
May 26, 2011
Posts
65
Reaction score
25
Nimeshtakiwa mahakamani kwa na mtu ambaye nilimkopa pesa kwa makubaliano ya kurejesha na riba ya 30% mwezi wa kwanza nikamlipa riba tu. Mwezi wa pili baada ya kuona sijamlipa riba yake + hela niliyomkopa, akaamua kuja kuchukua dhamana nyumbani.

Imepita miezi 10 ameamua kunishtaki mahakamani kuwa bado ananidai. Na hatua zote kuanzia kuchukua hela hadi yeye kuchukua dhamana hakuna mahali popote tulipoandikishana.

Naomba mwongozo wa kisheria tafadhali.
 
Kama hakuna mlipoandikishana therefore hakuna kesi.
 
Kisheria hapo utamlipa kwani makubaliano ya mdomo pia ni mkataba
Kama ana mashahidi wa kudhibitisha hilo.
Ila suala la riba hakuna sheria inamruhusu mtu kukopesha kwa riba kama siyo taasisi ya kifedha, hivyo mahakama itakuamuru umlipe kile ulichokopa tu, bila riba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…