Babu Kijana ,
Heshima yako!
Nina machache yakudokeza kuhusiana na gari uliyoitaja hapo juu.
Japo hujadadavua haswa ni yenye ukubwa upi wa cc ambao unahitaji
Maana ikumbukwe kwamba, gari hizi zina aina mbili ya engine yaani 6 Cylinders yaani 2,990CC = 3,000CC [3.0]
4 Cylinders yaani 2,290CC = 2,300CC [2.2]
6 Cylinders
ni chache sana ukilinganisha na 4 Cylinders hapa kwetu. Kwa sababu haswa gari hizi ni kwaajili ya watu wa safari ndefu za mara kwa mara, sio gari rafiki sana na safari za ndani (town trips) kwa sababu ina power kubwa na speed vile vile, vitu ambavyo vinachangia utumiaji mkubwa wa mafuta. Kwa wastani, inatembea kilometers 9 kwa Litre. (9KM/L)
4 Cylinders 2,290CC [2.2]
Hizi zipo common sana hapa mjini, na ndio wengi wanazipenda, asilimia kubwa ya hizi ulaji wake wa mafuta hua ni mdogo ukilinganisha na yenye 6 Cylinders kwa wastani hutembea karibia 11 kilometers kwa litre (11km/L)
Haswa hii imelenga kwa matumizi ya ndani (town trips) na sio rafiki sana kwenye kusafiria.
Jambo jingine,
Ambalo nadhani ungepaswa kuelewa ni kwamba, Toyota Harrier na Toyota Kluger ni kitu kimoja.
Yes, ni kitu kimoja, ni kitu kile kile. Unapotaja Toyota Harrier ni sawa unakua umetaja Toyota kluger.
Yaani this is in the sense that it’s only the body design, logo and name that were changed iliku-communicate the difference between the two vehicles.
Otherwise, haya magari (Harrier & kluger) yanatumia almost the same parts na the two engines give the same power output while exhibiting a high fuel consumption regimen.
Hitimisho :
Toyota Harrier na kluger, ni gari ile ile, tofauti kati yake na harrier ipo kwenye muundo wa design.
Na walifanya vile makusudi wakitarajia kwamba, sio wote wangependa muundo wa harrier jinsi ulivyo.
Lakini ukiachilia hapo, Toyota Harrier and Toyota Kluger are actually the same vehicles yenye the same engines type na capacity, the only difference between them being their outward designs.
Otherwise mechanically, and as far as interior design is concerned, you are dealing with the same vehicle.
Kuhusu kikokotozi cha tra,
Kwa Harrier ya 2004
Kwa mujibu wa calculator ya TRA
Used Motor Vehicle Valuation System - Used Motor Vehicle Valuation System.
Ni Tzs 11,977,000
Na ya 2006
Used Motor Vehicle Valuation System - Used Motor Vehicle Valuation System
Ni Tzs 12,669,000/=
2004 Toyota Kluger, kwa mujibu wa website ya TRA
Used Motor Vehicle Valuation System - Used Motor Vehicle Valuation System
Ni TZS 10,420,000/=
Na ya 2006 kwa mujibu wa TRA ni
Used Motor Vehicle Valuation System - Used Motor Vehicle Valuation System
Ni TZS 12,103,000/=
Zingatia :
Unapaswa kuwa na ziada ya angalau TZS 800,000/= Ili iweze ku cover gharama zingine zitakazo ongezeka , pia malipo ya bandarini, shippingline na wakala atakae kutolea gari lako. Itakua humo kwenye hiyo ziada (800,000/=)
Pia kwa sheria mpya ya sasa, gari zote inspection inapaswa kufanyika hapa hapa nchini , hivyo watakutoza pia gharama za inspection.