Naomba nisaidiwe namna ya kutengeneza cake ya kawaida

Mbwambo

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2008
Posts
625
Reaction score
94
Wana jamii nimepata mengi sana kwenye JAMII FORUMS na nina imani hata hili wapishi au Chef wa Jamii forums atanipatia
NATAKA NIWE NATENGENEZA BIRTHDAY CAKES KWA FAMILIA YANGU MWENYEWE
ASANTE
 
hii hapo sasa ila ni kizungu sasa itabidi ukomae tu mkuu...

 
kwa ninavyopika mimi keki.

ingredient:
mayai sita {tatizo la mayai mengine yanakuwa na maji mengi} kiurahisi chukua kikopo cha siagi robo kilo.hiyo siagi iweke kwenye bakuli lako.

na sukari ipimie kwenye hicho hicho kikopo cha siagi ila isijae mpaka juu.ichanganye pamoja na siagi.kama una mashine yako ya kusaga saga,mpaka ilainike.hicho hicho kikopo chako cha siagi,tia mayai yako.ila yasijae mpaka juu.mwaga kwenye huo mchanganyiko wa siagi na sukari.

saga wee,mpaka unakuwa uji mzito.hicho hicho kipimo chako cha siagi,tia unga wako wa ngano mpaka juu
mwagia kwenye ule mchanganyiko wako,tia baking powder kijiko kimoja cha chai.
unatia flavour yoyote unayopenda kama vanila au rose,au ya machungwa au ya mananasi.kila mtu na test yake.nusu ya kijiko chs chai.

unachukua mwiko wako,unachanganya{hapo hautumii mashine}unachanganya kwa muda kama wa dakika 2.{umemaliza}

unapaka sufuria lako mafuta kidogo.unakata karatasi lako ambalo liko plain,shape ya sawa na chombo unacho bake keki yako.unaiweka ndani.

unatia mchanganyiko wako.{mimi hupendelea rangi 2,ya chicklate na ya kawaida}kama unataka keki iwe kati kati ina rangi.unachukua mchanganyiko wako kidogo,unautia kwenye bakuli,unachanganya na cocoa.ukimaliza.mchanganyiko wako mweupe unautia chini mwanzo halafu katikati unaweka mchanganyiko wako wa rangi ya cocoa na juu unamalizia mchanganyiko wako mweupe.unaweka kwenye oven.wakati vkeko ipo ndani ya oven utasikia harufu nzuri ya kunukia.na ukitaka kujua keki imeiva katikati unachukua kijiti kikavu unakiingiza katikati.kijiti kikitoka kikavu,maana keki imeiva.
 
acha nikumbuke....... Keki ya fasta fasta.....

- Unga, siagi, sukari (kumbuka kipimo cha siagi na unga ni half fat to flour)
- mayai 4 au it depends na ukubwa wa keki
baking powder
vannila (vitone vichache), kama huna vanila kwangua ganda la kijani la limao (hapa una grate, hii ni kuondoa shombo na kutia harufu taaamu)

- changanya siagi na sukari koroga mpaka iwe nyeupe flani (ni vyema kama una mashine itakua fasta, kama huna bakuli kubwa la kioo na mwiko bapa vinahusika - hii niliitumiaga sekondari kwenye kipindi cha cookery)
tia mayai mix
tia vanila/maganda uliyograte ya limao mix
unga uchanganye na baking powder then mix
kama una zabibu au vikorombwezo (sometimes maziwa kwa mbaaali sana inategemea na mbwembwe zako), mix

paka baking tins zako siagi, hii huzuia keki kuganda kumbuka hapo oven iwe ushawasha
weka mchanganyiko wako
bake mpaka iiwe.....

Kuhakikisha keki yako imeiva vyema chukua palate knife dumbukiza, ikitoka clear jiandae kuidecorate

sijui nimeeleweka , i hope sijaacha kitu
 

asante sana nimekuelewa barikiwa
 

Mkuu badili tabia yaani ni umekimbia kiasi kwamba kuna baadhi ya details zinamiss so without hard feelings allow me to have them shared with other JF members.
Back to the topic, tutaanza na mahitaji then procedures and lastly heat specificatios.
Mahitaji;

1. EGGS .............................. 5
2. SUGAR ............................ vijiko 4 hadi 5 vya chakula
3. Siagi......................... .......¼ Kg ( hata ya 100g may work)
4. Vanilla....................... ......... Vijiko 2 vya chai
5.Unga wa Ngano.................. vijiko vya chakula10
6. Baking Powder................... vijiko vya chai 2
7. Zabibu kavu......................... ½ kikombe cha robo lita (si lazima)
NB; hayo mahitaji ni kwa jili ya keki ndogo kabisa hivyo basi vipimo vipo subjected to change depending na size ya cake utakayo.
Najua kwa wabongo tulio wengi tunakuwa na sukari zile nene za kawaida za kuunga kwenye chai ila na ni kikwazo kikubwa katika keki kuiva Barabara ila tuungane katika kipengele cha namna ya kutengeneza.
JINSI YA KUANDAA ;

  1. Weka sukari kwenye kinu na itwange hadi iwe powder kabisa ( kwa wale wenye common brown sugar kama za ilovo)
  2. Weka unga wa sukari kwenye bakuli lako la kukorogea ukichanganya na Blue band
  3. Changanya huo mchanganyiko wa sukari na Blue Band kwa nguvu hadi B/Band iwe nyeupe kabisa na sugar particles ziyeyuke kabisa.
  4. Weka mayai kwenye mchanganyiko wa B/Band na Sukari na koroga kwa nguvu hadi mchanganyiko uwe wa aina 1 (kama una blender itakuwa safi pia)
  5. Weka Unga wa ngano vijiko kama 5 kwanza then huku ukiangalia uzito wa mchanganyiko wako endelea kuweka unga katika huo mchanganyiko hadi vijiko 7 au nane then angalia uzito wa mchanganyiko. Mchangayiko usiwe mwepesi sana au mzito sana (kwani ikiwa nzito sana haitaiva vizuri katikati ). Koroga kwa nguvu hadi mchanganyiko ushikane vizuri na kusiwe ma mabonge yoyote yale.
  6. Weka B/powder yako na endelea kuchanganya (ni vizuri katika hii hatua ya mwisho hata kama una blenda ukakoroga kwa mkono katika bakuli ili mchanganyiko uwe vizuri/ichanganyike vizuri.
Wakati huo huo kama unatumia mkaa basi moto wako uwe tayari na umewaka vizuri au kama unatumia oven basi uwe umewasha oven kama dakika 5 kabla ya kuanza kuoka keki yako.
HEAT SPECIFICATION
Washa oven yako joto liwe nyuzi 150, ila kwa mkaa hakikisha kuwa moto sio mkali sana au joto halipo chini sana ila la wastani. Kama moto ukiwa mkali haitaiva ila itababuka tu juu juu na kama ukiwa ni mdogo basi keki haitaumuka wala kuiva vizuri.
Baada ya dakika 15 au 20 basi angalia kama keki yako imeiva , Jinsi ya kujuwa kama keki ipo tayari ni kuingiza kijiti kwenye keki na kikitoka na mchanganyiko unao nata ujuwe bado, ila kikitoka kikavu basi keki yako ipo tayari, pia hata rangi ya nje utaiona imebadilika…
Enjoy!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!:smile:
 

Mkaa unawekwa juu na chini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…