Inategemea na makubaliano ndani ya mkataba. kuna mikataba mingine ina kipengele ndani kinachosema "Yoyote atakae vunja mkataba huu, atamlipa mwenzake fidia yenye thamani ya mwezi mmoja tu/mshahara wa mwezi mmoja mbele".
Mingine unakuta ina kipengele "Atakae taka kuvunja mkataba huu, ni wajibu atoe NOTICE ya siku 7/masaa 24" n.k.
Kwenye kipengele cha kulipana mshahara wa mwezi mmoja mbele, hapa iwe mfanya kazi au mwajiri akiuvunja basi atamlipa mwenzake mshahara wa mwezi mmoja.
Mfano,
Tuseme "wewe" ni mwajiriwa wa JF (mfanya kazi) halafu JF ndio mwajiri wako, ikitokea wewe umepata kazi sehem nyingine yenye maslahi mazuri zaidi, halafu mkataba wako wa JF una miezi 10 mbele, ila hichi kipengele kipo katika mkataba wenu. Basi wewe utamlipa JF (Mwajiri wako) thamani ya mshahara wako wa mwezi mmoja. Na kama yeye akitaka kuvunja huo mkataba nae atakulipa wewe mshahara wa mwezi mmoja.
Kuna mikataba mingine ina kipengele cha kulipana mpaka "thamani ya mwaka mmoja". Inatofautiana na makubaliano baina ya MWAJIRI na MWAJIRIWA.