Naomba niweke wazi kwa wale wanaodhani ya kwamba hela iliyopo NSSF ni ya Serikali

Naomba niweke wazi kwa wale wanaodhani ya kwamba hela iliyopo NSSF ni ya Serikali

TUPAMBANE

Member
Joined
Jan 25, 2021
Posts
62
Reaction score
88
Habari,

fedha anayokwatwa mwanachama wa NSSF siyo ya serikali bali serikali inaisimamia tuu mifuko hii. hii fedha ni fedha ya wanachama.
Nashindwa kuelewa pale Mtu anaposema watanzania tunapenda vitu vya bure. Naomba nikuelimishe kidogo wewe unayesema tunapenda vitu vya bure.

Kama kazini kwako au ulipoajiriwa unalipwa laki saba kama ndio mshahara wako NSSF wanachukua kutoka kwenye mshahara wako kiasi cha asilimia 10 ambapo itakuwa ni elfu 70 halafu mwajiri wako pia anakuchangia wewe mfanyakazi wake asilimia 10 ambapo itakuwa jumla 140,000 sasa hiyo hela ndio itakuwa inapelekwa NSSF kila mwezi hivyo kama utaongezewa mshahara basi hivyo hivyo kiwango cha fedha itakayopelekwa nssf itaongezeka ila asilimia ni kumi ya mshahara wako.

Sasa hicho kiwango cha mshahara kama utafanya kazi kwa miaka 15 ni kwamba unachukua 140,000*miezi 12 halafu utakayoipta ndio unazidisha kwa miaka 15. mfano (140,000*12=1,680,000 sasa hii unazidisha kwa 15=25,200,000 hivyo unapata zaidi ya milioni 25 kwani hapo nimepiga bila nyongeza ya mshahara hivyo kama mshahara utaongezeka utapata fedha nyingi zaidi.

Tuje Kwa upande wa serikali, serikali inafaidika vipi na mshahara wako kama kodi? serikali baada ya kukata NSSF yako maana kama ulikuwa unapokea laki 70000 watatoa hapo hiyo asilimia 10 ya nssf (700000-70000=630000) hivyo hiyo 630,000 serikali inachukua hapo kiasi cha shilingi elfu 44500 kila mwezi kama kodi.

Kwa hiyo take home yako inakuwa 585500 (700000-70000ya nssf-44500 ya kodi ya serikali=585500) sasa hiyo 585500 ndio unaenda nayo nyumbani sasa hapa tunaanza kuifanyia kamchakato nikikosea mtanirekebisha

1. Kodi ya nyumba chumba na sebule sehemu za kawaida 80,000
2. Matumizi ya nyumbani kama matumizi ya kawaida 300,000
2. Umeme kwa vile utakuwa umepanga na luku mnashare 10,000
3. Maji ya kutumia kwa mwezi 10,000
4. Nauli ya kwenda kazini tupigie gari moja 800*22= 17600
5. Maji ya kunywa kazini 800*22= 17600
6. Chakula kazini 2000*22 44000

JUMLA NI KIASI CHA 479200 JUMLA
Hivyo unabakiwa na kiasi cha elfu 106300
sasa hapa tuje kwa matumizi ambayo nikiweka hapa utalia
1. Ada ya watoto hapa kama watakuwa wanahitaji nauli mimi sijui wewe wajua
2. Mjomba wangu yuko Mjini ngoja nimwombe fedha hao waliokusomesha utakuwa unawajua wewe mimi na Samiha Suluhu hatuwajui
3. Kumetokea tatizo kijijini kwenu ngoja wakupigie simu mimi siju wewe wajua
4. Bado kama hujaoa kuna wale tuma na ya kutolea unawajua wewe

Sasa hapo mwaka wa 15 kuelekea wa 16 unasimamishwa kazi au unafukuzwa kazi bosi amekuchoka au kutokana na kusumbua sumbua na visababu kwamba naumwa leo siji kazini kumbe umeenda kufanya kibarua sehemu nyingine upate ada ya mtoto au utume mchango wa rambirambi kijijini hivyo bosi anachoka na ruhusa zako anakuandikia poor performance hivyo tunakufukuza kazi. Unarudi kitaa hueleweki unasema ngoja nizame NSSF kuchukua mafao yako ukafungue kiduka unaambiwa hela haitoki mpaka ufikishe miaka 60 hapo unamiaka 35.

Keshokutwa baba mwenye nyumba anakuja na bili zote za kodi umeme maji, kodi sasa kwanini usichanganyikiwe ukaitelekeza familia na kukimbia? kwanini usisalimie michongoma? maana unaweza ukawa unatembea unaona kisiki cha mchongoma unaanza kusalimia habari ya hapo jamani. Kumbe kisiki cha mchongoma

Nimalizie kwa kusema NSSF sio msaada bali ni jasho lako.

SAMIA SULUHU SHUGHULIKIA MAFAO YA NSSF
 
Kweli kabisa mi naumia jamani pesa yangu wameizulia huu mwaka wa nane unaenda naambiwa hadi nifikishr miaka 60 ndio nitapewa na hapa sina ajira yoyote nakula kwa kubangaiza wakati hela yangu IPO tu imekaa huko. Watuonee huruma na hii corona watupe tuendeleze maisha yetu
 
Write your reply...Msitu ni ule ule kunyonya wengine ndiyo kanuni ya watawala usitegemee makubwa kutoka kwa huyu mama malalamiko ya watanzani hayajawahi kupatiwa ufumbuzi sahihi miaka 60
 
....... Hela haitoki mpaka ufikishe miaka 60 na hapo una miaka 35.....
😂😂😂
 
Akiweza kulifanyia hili kazi sijui atakua mungu mtu hata duniani, kwa maaana kinachofanyika sasa hivi ni utapeli muajiliwa anakatwa PAYE inafika Mpaka 18% based on your salary, ambayo ni kodi Yao at the same time unakatwa. NSSF ambayo hailudi si kama hapo awali sasa ni wizi huo na dhurma?

Mama tunakuombea mwenyezi mungu akulinde na akupe hekima na busara Ya kuliangalia hili la Dhulma , wabunge wangekua wanakatwa vyote hivyo wangepiga kelele
 
Aisee ulichosema ni kweli, wengine tulibahatika kufanya kazi kwenye kampuni miaka tofauti tofauti,hakuna hata mia unayopewa tangu tutoke huko.... wengine hata hiyo 30 tuu bado mpaka tufike 60 ni leo na magonjwa haya ya moyo kukata umeme kwelii???
 
Naomba kujuzwa hivi ikitokea mwanachama ambae yupo nje ya ajira akifariki kuna fao lolote familia itafaidika?
 
Kweli kabisa mi naumia jamani pesa yangu wameizulia huu mwaka wa nane unaenda naambiwa hadi nifikishr miaka 60 ndio nitapewa na hapa sina ajira yoyote nakula kwa kubangaiza wakati hela yangu IPO tu imekaa huko. Watuonee huruma na hii corona watupe tuendeleze maisha yetu

na hiyo ukifika miaka 60 wanakupa na riba au wanakupa kama ilivyowekwa?

kwa sababu elfu 50 ya leo sio sawa na elfu 50 ya miaka 30 ijayo
 
Umejitahidi sana. Ila kwenye calculations za kiasi cha kulipwa na NSSF umekosea. Kuna formula maalum
 
na hiyo ukifika miaka 60 wanakupa na riba au wanakupa kama ilivyowekwa?

kwa sababu elfu 50 ya leo sio sawa na elfu 50 ya miaka 30 ijayo
Unapewa kulingana na thamani ya fedha ya mda huo ndo maana hela zinazo katwa na mifuko ya hifadhi za jamii
Zinapelekwa kwenye investment na kila mwanachama atapata investment return.
Note sio kile unacho save ndo utapokea utapokea baada ya investment return.
Unakuta ulisave 15m lakin ukistaafu unakula 30m
 
Hawatakuelewa..

Tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana...
 
Back
Top Bottom