Naomba nondo kuhusu gari aina ya Subaru Forester XT

Ukitaka kujua gari nzuri na mbaya ni ipi fanya hivi:

Nenda kwenye pages za used cars utakuta madalali wanauza gari za hovyo zinauzwa zikiwa mpya namba DT, DR, DV kwa bei chee na gari za maana zinauzwa na namba A au B na ukikuta C bei haishikiki karibu sana na ya kununua jipya.

Ikusaidie hiyo.
 
Well. Binafsi napenda magari yenye fewer kms nikiwa nainunua.

Higher mileage ni near disposal.

Anaenunua gari na 50k km anapotential ya kutumia gari yake for the next 200k kms endapo ataitunza vizuri.

Ila mwenye kununua gari yenye 150k km sidhani ana potential ya kuendesha for the next 150k km bila cranks.
 
FYI hizi used cars....una hatari zaidi ya kuuziwa fake mileage iwapo utanunua hizo zenye 50k kuliko anaenunua ya 100k+. Mbaya zaidi unaendesha huku unaamini ni 50k wakati kiukweli ni 150k. Wauzaji washajua akili za madereva wanaabudu digits kwahio wanaenda sawa nao. Hizo 40k,50k nyingi sana za uongo.
 
From Japan au hapa bongo?
 
Ni kosa sana kununua gari kwa kuangalia watu wanasema nini,unaeza kuta anaekosoa unachotaka nunua yeye hana hata pikipiki,anaeleza matamanio yaliyojaa kisirani na nia ya tukose wote,nunua gari kulingana na matumizi unayotaka litumia na hela yako,
Kuna watu waliokuwa na level ya kumiliki ist waliingia mkumbo wa kutonunua sababu tu kuna mkuu alilewa sifa akazitusi,lkn ukweli ukabaki kuwa ist ni gari nzuri kwa maisha ya kawaida ya mtu wa kawaida na ni rahisi kulimudu,
Kuna mtu hela ya kuunga unga anataka nae eti kushindana kununua gari kwa fashion badala ya hali halisi na tumizi,wapo watu anaweza badili gari kila mwaka,utashangaa mwenzangu na Mimi nae anafuata mkumbo wa fashion wakati mfukoni miungo mitupu,
Nunua gari kulingana na matumizi,uchumi wako na mazingira,
Fashion acha akina ronaldo na myweather washindane huko.
Usibabaike chukua harrier yoyote
 
Sitegemei kukuta gari ya 2009 and below iwe na 50k kms. Hata kama zipo ni za kubahatisha sana.

Ila kuna possibility kubwa gari ya 2015 na kuendelea ikawa na 60k kms.
 

Daah madalali hua wakipata wasukuma wa dizaini yako hua wanafurahi kichizi.
 
Nakubali mwamba! Mie gari yangu ni 200K+ ila iko njema mno kiasi kwamba huwezi dhani ina hizo kms! Gari ni matunzo tu!
 
Dah.. umenirudisha njiani mwanangu maana xt zilivyopondwa humu hadi nikawa nimekata tamaa
Hadi sasa kichwani nimepanga kununua xt lkn manual au escudo new model basi hayo mengine nawaachia ninyi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah.. umenirudisha njiani mwanangu maana xt zilivyopondwa humu hadi nikawa nimekata tamaa
Hadi sasa kichwani nimepanga kununua xt lkn manual au escudo new model basi hayo mengine nawaachia ninyi.

Sent using Jamii Forums mobile app

Siyo vibaya kuomba ushauri na kusikiliza then kuamua ni wewe. Ila ogopa sana ushauri usio na vigezo. Kauli kama achana na hiyo gari halafu huambiwi kwa nini ni za hovyo. XT kama unaipenda hivyo nunua, siyo gari mbaya. Kuna gari zina reliability issue, hii si mojawapo. Ila tambua tu gari yoyote yenye turbo especially hizi za miaka ya 2010 kushuka chini zinahitaji kuzingatia service. So kama huna mahitaji ya ziada, engine isiyo na turbo ni bora zaidi.
Escudo nayo gari imara, engine zake ziko simple na kama kawaida, zingatia service. Hazina reliability issue, especially kama utapata J20 na J24 engines
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…