NAOMBA SHERIA INAYOHUSU KODI ZA MAJENGO

NAOMBA SHERIA INAYOHUSU KODI ZA MAJENGO

Katali

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2016
Posts
861
Reaction score
695
Nakumbuka wakati fulani Mh.Waziri wa ardhi alitamka kwamba majengo ambayo hayajakamilika na hayatumiki kwa makazi hayalipiwi kodi, pia nilisikia Mmiliki wa Nyumba mwenye umri zaidi ya 60 pia hatakiwi kulipa kodi lakini pamoja na kumbukumbu zangu hizo leo nimeletewa barua ya madai ya kulipa kodi ya jengo wakati jengo langu hatakuezeka sijaweza! Mbaya zaidi wamempelekea mama yangu barua kama hiyo ambaye ni mjane na ni mzee wa miaka 70 ! Naombeni authority ili nijaribu kujinasua na kadhia hii.
 
Kwa elimu ndogo niliyonayo juu ya ardhi ni kwamba kodi ambayo ina msamaha ni kodi ya majengo kwa mtu mwenye umri kuanzia miaka 60.Mhusika unaandika barua kwa Kamishna Mkuu wa Mapato ukimwomba huo msamaha na uthibitisho wa umri wako.Pia kwa nyumba ambayo haijakamilika ujenzi wake haitozwi kodi ya jengo
 
Asante sana mkuu nimepanua wigo wa uelewa.
 
Back
Top Bottom