Naomba suluhisho ya meno, yanapukutika sana

Bakulutu

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2011
Posts
2,557
Reaction score
1,787
Habari wakuu, nimeshango'a meno 3 na sasa mawili tena yameliwa, mawili nimeziba, naona sasa nitapoteza yote. Naomba mwenye kujua tiba kamili na yenye mafanikio tafadhali.
 
Subiri waje wajuzi.

Hujawahi tumia dawa yoyote kuweka kwenye meno?
 
subir waje wajuzi.swali hujawahi tumia dawa yeyote kuweka kwenye meno??
Kuna dawa fulani hivi nilinunua pale feri kigamboni nikatumia kama siku 3..
 
Acha kula vyakula vya sukari na kama ukitumia ndani ya dakika 20 upige mswaki.

Mfano wa vyakula vya sukani ni biscuit(hasa hasa hapa pa biscuit), pipi, candy, keki na the like
 
Fanya mpango wa kuoata dentures tu.
Acha vyakula vya sukari,
Tumia dawa ya meno Sensodyne, na Listerine mouthwash all the time.
 
Tumia majivu ya jiko la mkaa kupigia mswaki. Yanasaidia kuondoa acid kwenye meno...
 
acha kula vyakula vya sukari na kama ukitumia ndani ya dakika 20 upige mswaki

Mfano wa vyakula vya sukani ni biscuit(hasa hasa hapa pa biscuit), pipi, candy, keki na the like
Na miaka kama 7 situmii hivyo vitu ila sielewi nini shida
 
Fanya mpango wa kuoata dentures tu.
Acha vyakula vya sukari,
Tumia dawa ya meno Sensodyne, na Listerine mouthwash all the time.
Sensodyne ndio natumia siku zote na vyakula vya sukari situu kabisa ata kwenye juice naweka kwa mbali saana
 
Sensodyne ndio natumia siku zote na vyakula vya sukari situu kabisa ata kwenye juice naweka kwa mbali saana
Tatizo ni ratiba yako ya kupiga mswaki.. Mara nyingi meno yetu yanakua masafi ndani ya nusu saa kwa siku nzimu muda mwingine wote meno yanakua ni machafu,kwa staili hiyo lazima ung'oe meno...please nisubiri kidogo nitakuja kukupa ratiba nzuri ili kuyaokoa meno yako
 
pata mbegu za mlonge glass 1 na chumvi mawe kijiko 1cha chakula.Twanga pamoja vilainike kisha weka ktk chombo chenye mfuniko halafu huo mchanganyiko TUMIA KUPIGIA MSWAKI MARA 2KWA KUTWA mf
asub na jion SHARTI USITUMIE MIDAWA YA MENO YOTE YENYE SUKARI NYINGI HUHARIBU MENO
 
Habari wa kuu, nimesha ngo'a meno 3 na sasa mawili tena yameliwa, mawili nimeziba, naona sasa nitapoteza yote naomba mwenye kujua tiba kamili na yenye mafanikio tafadhali.
Meno yanaoza au vip? Njoo inbox nikupe dawa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…