Naomba tafsiri wanasheria

CHUAKACHARA

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2011
Posts
12,357
Reaction score
6,424
Child act, 2009, SECTION 36 reads: Where the court has made an order on a biological father, such biological father shall assume the responsibility to the child in the same manner as may be in respect of a child born in wedlock and the child shall, subject to religious belief of the biological father, have such other rights devolving from the parent including a right to be an heir.

Je kifungu hicho hapo juu, kinapingana na sheria ya Sheria ya urithi ya India ya 1865 (ya serikali) inayosema: Kwa mujibu wa sheria hii watoto wa nje ya ndoa hawana haki ya kurithi isipokuwa kama kuna wosia na katika wosia huo wawe wamerithishwa mali.


Au sheria za kimila/ kidini zinazokataza mtoto wa nje ya ndoa kurithi! Hapo penye red tafsiri yake ni ipi?
Ni sheria ipi ita-prevail- ya kimila itawekwa kando, je hiyo ya India maana inatumika hapa!
 
written law ina prevail kk, na Indian law it can b used as parematilia in tz if our law dd not specify....wengine toeni views.
 
Where there is a conflict between customary law and statutory law, statutory law shall prevail. S.9 ya jala. In the probate act, i dont remember ni section ipi, it states something like where religious law is unfair or discriminative then it will be overrule. Go through the probate act.
 

Thanks a lot!
 
Mkuu sana CHUAKACHARA,katika taratibu za kisheria za nchini mwetu Sheria yoyote ya nje hutumika pale tu ambapo kuna kutojitosheleza kwa Sheria yetu/zetu juu ya suala fulani. Katika minajiri hiyo, Sheria ya Mtoto ya mwaka 2009 ndiyo hasa inayotumika kuhusu suala uliloliainisha.

Kulingana na kifungu ulichokidondoa, hakuna utata au kupingana kokote na Sheria yoyote ya Tanzania. Mkuu CHUAKACHARA, jambo hili lakufanya baba mzazi atajwe na Mahakama na papo hapo mtoto aanze kufaidi faida zakuwa na baba mzazi ni katika juhudi za jamii kuondoa mahangaiko kwa watoto wanaozaliwa nje ya ndoa.

Kimsingi, Sheria ya Mtoto niliyoitaja hapo juu imeleta mabadiliko makubwa katika masuala yamhusuyo mtoto. Ni Sheria ya kupigiwa mfano pamoja na kuwa na hitilafu za hapa na pale.

Hivyobasi, Sheria ya Mtoto ya mwaka 2009 ya Tanzania haipingani kwa namna yoyote na Sheria hiyo uliyoitaja ya India kwakuwa Sheria hizo mbili hazitumiki pamoja na kwa uzito sawa hapa Tanzania. Sheria zetu zaTANZANIA huanza kutumika kabla ya zote za nje.Asante Mkuu

Wakili Msomi Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
 
Last edited by a moderator:

Nashukuru sana Mkuu. Ufafanuzi murua. Naomba niulize zaidi kidogo kama sitaku-bore! Ina maana sheria imeruhusu uzinzi. Unaweza zaa nje bila woga. Kama sheria inamtambua mtoto, basi inaruhusu hata wakristo kuoa zaidi ya mke mmoja. One can argue that way! Huwezi kuwa na halali kutokana na haramu!- Usiku unafuatwa na mchana! Hata common sense inatuongoza hivyo!
Lakini wemeweka angalizo kuwa kama dini ya mhusika inakubaliana na hili-(katika kifungu nilichokinukuu. Naomba ufafanuzi wako!
 
Mkuu CHUAKACHARA, si vyema kusema kuwa Sheria ya Mtoto inaruhusu uzinzi.Uzinzi huruhusiwa na dhamira ya mtu binafsi. Kilichofanywa na Sheria ni kumlinda mtoto ambaye hana hatia yoyote juu ya kile kilichotokea ima kiwe cha kizinzi au la. Hakuna dini hata moja iruhusuyo uzinzi. Hakuna pia dini ya kikristo inayoruhusu ndoa ya wake wengi.Ni dhamira mbovu tu za watu. Si Sheria iruhusuvyo.
 
Last edited by a moderator:
Wadau naona kuna haja ya kuput records clear hapa India Succession Act ya mwaka 1865 sio foreign /international law ka wadau wengine wanvyoifikiria hii sheria inanFTguvu sawa sawa na sheria zingine zilizotungiwa Tanzania maana hii sheria tumeingiza kwny mfumo wetu wa sheria itumike ka other domestic laws ndio maana amendments au revision zinazofanywa India haziaffect hii tunayoittumia Tanzania ya kwetu bado iko vile vile since we adopted it
 
Wadau naona kuna haja ya kuput records clear hapa India Succession Act ya mwaka 1865 sio foreign /international law ka wadau wengine wanvyoifikiria hii sheria inanFTguvu sawa sawa na sheria zingine zilizotungiwa Tanzania ....
Ndio na mi nashangaa...! Unawezaje kusema Indian Succession Act of 1865 ni foreign law kwa Tanzania?

Section 14, J.A.L.A The Acts of the Governor-General of India in Council set out in the third column of the Second Schedule hereto (and hereinafter referred to as "the Indian Acts") and such amendment of or substitution for the same as was in force on 1st December, 1920 are, subject to the exceptions described in the fourth column of the said Schedule, hereby applied to Tanzania.


Where there is a conflict between customary law and statutory law, statutory law shall prevail. S.9 ya jala.
Duuh! Section 9 ya J.A.L.A inasemaje? Kuna kamba humu ndani sijapata kuona...

Section 9, J.A.L.A: "The provisions of the Acts of the Parliament of the United Kingdom described in the First Schedule hereto, as amended prior to the twenty-second day of July, 1920, shall apply to and have effect within Tanzania subject to the exceptions, adaptations and modifications set out therein."

Sasa we dada, hebu nionyeshe umepata wapi hicho kipengele cha "Where there is a conflict between customary law and statutory law, statutory law shall prevail"?????

Basically the British and Indian laws which are enumerated in J.A.L.A sio sheria ya kigeni, zimesimikwa kuwa ni sheria za kibongo kama sheria zingine tulizojitungia wenyewe. Tukubaliane hilo above all. Kwanza sisi hatuna sheria yetu tuliyojitungia ya urithi, kwa mfano, sasa utasemaje sheria ya India haina nguvu kama sheria yetu? Yetu ipi?
 
There is a chance nimekosea the proper section sema there is a provision kwenye jala inayoongelea hiyo kitu. Just go through hiyo jala na kuna case laws. Its first year legal system. But its a trite law customary law can never prevail over and above statutory law.
 
Naona mkuu kwa chini umejipiga promo wakiki msomi wakati advocates act inakataza mkuu..touting hiyo mkuu sijui nimepatia mana nilisomaga long time kinoma
 
Last edited by a moderator:

Mimi nafikir ni katika kutoa matunzo tu ila maswala ya kurithi hiyo ni ngoma mpaka huyo born out of wedlock ajumlishwe kwenye wosia huu ni mtazamo tu
 
There is a chance nimekosea
sio "there is a chance nimekosea," umekosea, period! Hicho kipengele hakipo!

Just go through hiyo jala
Huwezi kunambia mimi ni "go through JALA" wakati wewe ndio umetoa kipengele potofu na umekiri hivyo. Wewe ndio uende ku "go through JALA..." ukaji enlight with the facts... Unatunga vipengele halafu unanambia mimi go through JALA, we vipi?
 
Reactions: SMU
Sijui ulikuwa na ma stress yako ulivyo andika hii post. Ushauri aombe mwingine, msaada nitoe mimi, kupanic upanic wewe.
I was just trying to the dude. Get a life
 
mkuu court inachofanya ni to strike a balance so hairuhusu unzinzi ila ndo ishatokea mtu kazaa nje lazima kuwe na kitu cha kuwasimamia hao watt af izo sheria za nje kama iyo ya india can be used only where there is a lacuna in our statute#regards
 
Naona mkuu kwa chini umejipiga promo wakiki msomi wakati advocates act inakataza mkuu..touting hiyo mkuu sijui nimepatia mana nilisomaga long time kinoma

Hiyo advocates act inakataza nini? Kutangaza huduma unazotoa au? Na kama inakataza kutangaza huduma unazotoa, watu watajuaje sasa kuwa wewe ni 'wakili msomi' na unatoa huduma hizi na zile?
 
written law ina prevail kk, na Indian law it can b used as parematilia in tz if our law dd not specify....wengine toeni views.

And what the flipping hell is "parematilia" in common modern-day parlance?
 

mkuu sisi tumerisi sheria zile na kuzifanyia amendment,baada ya hapo ndo zikawa zetu. Sasa ikitokea LACUNA in our laws ndo apo Tutarudi kwenye Indian Laws
 
hahaha I am enjoying the manner in which arguably young,naive lawyers and wanna-be advocates wrangle in here..
Surely, if the arguments are anythng to go buy,and save for one or two guys-most of you have a long way to go.
 
Reactions: SMU
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…