Habari wana jamvi..
katika pitapita zangu nimekutana na neno RAGHBA, ni neno la kiswahili lakini nimeshindwa kulielewa vizuri zaidi hasa mahala pa kulitumia.
Tafadhali wataalamu wa lugha naomba mnieleweshe..
Raghba ni MAPENZI uliyonayo juu ya jambo fulani au kitu.mfano wewe ukiwa ni mpenzi sana wa lugha ya kiswahili basi twaweza sema kuwa UNA RAGHBA NA KISWAHILI. kimatumizi yani ni kukipenda kitu au jambo.mapenzi yanayozungumzwa hapa si yale ya mtu na mwandani wake(MAWADA)