DOKEZO Naomba TAKUKURU iwachunguze Viongozi na Wafanyakazi wa NSSF Dodoma maana binafsi nahisi Kuna viashiria vya Rushwa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Milonji

Senior Member
Joined
May 26, 2022
Posts
166
Reaction score
510
Wakuu habari za Leo?

Naomba kwanza kusema ya kuwa Mimi nilikuwa ni Mwajiriwa wa Kanisa la Anglican Tanzania na nilikuwa nikifanyia Diocese ya Central Tanganyika (DCT) pale Dodoma.

Nimefanya nao KAZI kwa muda mrefu takribani Miaka 15+ kwa mkataba mfupi mfupi mpaka pale wao (DCT) walipoamua kutoniongezea Mkataba kwa sababu mbili tatu (ila sijafukuzwa KAZI).

Baada ya kuhitimisha muda wangu walinipatia haki zangu ikiwemo barua na cheti cha Utumishi.

Baada ya siku kadhaa nikaamua kwenda NSSF pale Dodoma ili kujua namna ambavyo nitapata mafao yangu.

Nilipofika pale na kuomba statement nikakuta Mwajiri wangu hajalipa michango yangu kwa takribani Miaka 3.

Nilipowauliza NSSF kwa nini Mwajiri hajalipa michango yangu na nilikuwa nikikatwa Kila Mwezi kwenye Mshahara wangu. Wao wakasema hawajui sababu iliyomfanya Mwajiri ashindwe kulipa na sipo peke yangu ambaye michango yangu haijawasilishwa.

Binafsi niliwaambia ya wengine hayanihusu, nahitaji kujua sababu ya kutowasilishwa kwa Michango yangu. Hili swali walishindwa kunijibu na badala yake nikaelekezwa kwendakumuona Mneja Rasilimali Watu (HR).

Nilipo onana na HR yeye aliniambia Suala langu amelipokea na linashughulikiwa na baada ya wiki mbili litakuwa tayari. Baada ya wiki mbili nilirudi NSSF lakini Michango ikawa Bado haijawasilishwa.

NSSF wakanirudisha tena kwa HR japo awali nilikataa maana niliwaambia wajibu wa kukusanya Michango yangu ni wao. Baada ya malumbani kwa muda nikakubali kwenda kwa HR nako hadithi ikawa ni ile Ile ya njoo Kesho.

Nimefuatilia NSSF na DCT kupitia HR mpaka nikachoka. Siku Moja nikaona isiwe shida Bora nikaonane na Baba Askofu Dk. Chilongani (Samahani kama nimekosea jina). Nikapewa siku ya kuonana naye. Kitu cha ajabu Ile siku nilipoenda ofisini kwake ili nizungumze naye nikazuiwa kwa madai kuwa wageni tupo wengi. Hivyo nikapangiwa siku nyingine.

Nilipoenda mara ya pili Hali ikawa ni ileile. Kiukweli nilipatwa na hasira sana, naamini yule Sekretari aligundua Hilo maana nilitaka kuingia ofisini kwa Askofu ki-nguvu.

Nikapewa nafasi ya tatu hiyo siku nilisema ama zake ma zangu. Nilipofika nikaambiwa subiri kidogo, nikasubiri huku nikiwa na sura ya kikauzu kwelikweli. Mara akaitwa aliye Nyuma yangu ili aingie, Kiukweli uvumilivu ulinishinda yule Mzee (sijui ni Mchungaji), nilimzuia na tukaanza mabishano kati yangu na Sekretari. Baada ya muda niliingia kibabe. Duuuh.... nafika mle ndani Baba Askofu hayupo.

Nikatoka kwa haraka ili nikamalizie hasira zangu kwa HR. Nafika Ofisi ya HR naangalia kwenye ngazi namuona Baba Askofu anashuka ngazi (baadae nilikuja kubaini kuwa kuelekea Ofisi ya Baba Askofu na pale kwa Sekretari kuna CCTV Camera, hivyo anapoona hali si shwari anapitia mlango wa dharura na kuondoka). HR nilipoingia kwake sikumkuta japo mlango ulikuwa wazi.

Nikaamua kwenda NSSF kuwapa taarifa, wao wakaniahidi kufuatilia michango yangu.

Tangu wakati huo mpaka sasa mafanikio hakuna kabisa. Kila nikienda ni danadana mwanzo mwisho.


Sasa ninajiuliza;
1. Kama NSSF tawi la Dodoma wanao wajibu wa kuhakikisha Mwajiri wangu anapeleka Michango yangu. Kwa nini hawafanyi hivyo?.

2. Je Diocese of Central Tanganyika (DCT) inawapa nini hawa Viongozi na Watumishi wa NSSF Dodoma mpaka wanakuwa hawafuatilii haki ya Mfanyakazi?.

3. Kwa nini Diocese of Central Tanganyika (DCT), hawapelekwi mahakamani ili walazimishwe kulipa deni husika?.

Naomba TAKUKURU iwachunguze Viongozi na Wafanyakazi wa NSSF Dodoma maana binafsi nahisi Kuna viashiria vya Rushwa.

Kwa masikitiko nawasilisha.
 
Duu pole sana mkuu, mimi nakuombea tu upate haki yako kwa wakati na bila usumbufu mwingine zaidi ya huo ambao umeshaupata .
 
Mimi kwa uelewa wangu mdogo wewe ndio unatakiwa ufunguwe kesi ya madai hayo, maana kama wamekupa stahiki zako na termination letter itwafunga tu na pesa yako utapewa, kosa analo mwajiri wako na sio NSSF, cha muhimu rudisha feedback hiyo na uombe wakuelekeze uanzie wapi pesa yako itawekwa yote
 
Huwezi kuangalia kama Kampuni inaingiza mafao yako nssf kila mwezi badala ya kusubiri miaka kupita au kuacha kazi?
 
Jukumu la kufuatilia michango ya mwanachama ni jukumu la NSSF. Kwa hali ya kawaida huwezi kwenda kumdai michango mwajiri huenda akakudhuru etc. The same situation ipo NSSF Mbeya, kuna kiwanda kinaitwa Knew Kingdom kipo kata ya Kalobe Mbeya Mjini. Mwajiri hajapeleka michango ya wanachama tokea 2014 hadi mwaka jana alipoamua kusitisha shughuli ya uzalishaji Pombe. Watu wanateseka wao wamekaa ofisini wanakula kiyoyozi…. Hii nchi maskini wanateseka sana
 
Unajisimbua ndio maana watu wameupuuza huu uzi wako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…