naomba tuchangie uzoefu kuhusu ujauzito

naomba tuchangie uzoefu kuhusu ujauzito

Mocrana

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2011
Posts
536
Reaction score
122
ujauzito umenibadili si tu maumbile ya mwili bali na hisia mwanzoni sikuwa na wivu kiasi hichi kwa mume wangu lakini tangu nipata ujauzito nimekuwa na wivu sana na nampenda sana mume wangu, najitahidi niushinde lakini wapiii, inafika wakati nahisi namboa huyu baba kijacho, wenzangu ilikuwaje?
 
Mocrana, bora weye unampenda mumeo, kuna binti jirani yangu, yeye anadai hampendi mumewe wala hataki kumsikia :confused3:. Ila jaribu tu kuongea na mumeo aelewe, wengi huwa wanaelewa. Otherwise, enjoy every moment of your pregnancy
 
Last edited by a moderator:
Uzoefu wangu niliona hayo ni mabadiliko ya hormone wakati wa ujauzito,wengine unakuta wanakuwa na hasira,wana tapika au kichefuchefu,wanakuwa na hamu sana kumega mkate(tendo la ndoa) au hamu kupungua kabisa kuliko wakati wakiwa hawana ujauzito,kupenda sana and viceversa.tabia hizi zinaweza kuisha kadri mimba inavyoendelea kukua au ikaisha pindi mwanamke ajifunguapo.

Chukulia ni hali ya kawaida itaisha.
 
Kwanza nakupa hongera sana kwa hali uliyonayo. Pia ni kawaida sana tena sana kwa mjamzito kuwa na mabadiliko mbalimbali ya katika mwili wake, tena mshukuru Mungu unampenda, ukimchukia inaweza kufikia stage mwanaume anashauriwa akupeleke kwao hadi ujifungue!

Kwa mwanaume aliyefundwa hawezi kuboreka na hali yako kwani huwa wanafundishwa katika mafundisho ya ndoa kwamba hali kama hiyo inaweza kutokea iwapo mke wake amepata ujauzito.

Hivyo, usihofu ni hali ya kawaida tu, itaisha ukijifungua
 
hongera mwaya, nimepita tu jamani humo simo wakati ukifika namm nitashare uzoef wangu, all the best bibie
 
ahsante, aisee ni experience nzuri, mana kuna challenge nyingi lakini mwisho wa siku ukifikiria kuna kiumbe chenye uhai ndani yako unasahau yote, its not easy but its worth it.
hongera mwaya, nimepita tu jamani humo simo wakati ukifika namm nitashare uzoef wangu, all the best bibie
 
conglatulations.....that must be a baby girl.
 
Back
Top Bottom