Naomba tupeane uzoefu wa kuishi nyumba moja na mama mkwe baba mkwe mashemji

MRS GINOLA

Member
Joined
Jan 6, 2017
Posts
50
Reaction score
61
habari zenu wadau mm na baba watoto tulikua tunaishi ktk nyumba ya kupanga kwa muda wa miaka minne sasa ila anataka tukaishi kwao kwa kua kidogo kodi imepanda ili tusave tuweze kuanza kujenga makazi yetu sasa jamani naomba mnipe uzoefu wa kukaa na mama mkwe baba mkwe mashemeji na mawifi ndani ya nyumba mm nikiwa nina watoto wawili wadogo 3 years na 1 year mm ni mfanyakazi naenda kazini asubuhi jumatatu hadi ijumamosi siku yangu ni moja tu jumapili kiukweli mm sipo comfortable kuenda kulundikana kwenye nyumba moja yaani nipo nafuraha nikiwa naishi kwangu. si kama siwapendi ndugu wa mume lakini sipo comfortable. hebu nipeni mawazo yenu juu ya hii ishu.

naomba mwenye lugha ya kejeli afunge mdomo wake
 
sio wazo baya as long mna malengo ya kujenga
ingawa ina changamoto bt kila kitu kinahitaji sacrifice

Sent from my TECNO-J8 using JamiiForums mobile app
 
Mwambie mumeo aache kuogopa maisha kwani kuna nyumba zenye gharama nafuu mwaweza kwenda kukaa huko kuliko kwenda kuishi ukweni. Usithubutu kwenda kuishi ukweni kwa kigezo cha kutaka kujenga, mwambie mwenzio akubaliane na changamoto za maisha mwaweza kuwa juu ama kushuka chini ila kikubwa ni kupambana.
 
sio wazo baya as long mna malengo ya kujenga
ingawa ina changamoto bt kila kitu kinahitaji sacrifice

Sent from my TECNO-J8 using JamiiForums mobile app
kwa kweli changamoto ni nyingi unajua ss wadada ambao hatupo home muda mwingi siku ukikaa hapo unaweza kupata mastrees ukaudhika na najiona kabisa ninakwenda kuface stress kwa kweli mkitaka mpendane na kupatana na mawifi na wakwe na mashemeji ni mkae mbalimbali muwe mnatembeleana tu kwa kweli daima mtapendana
 
kabisa yaani kwa kweli hii ni changamoto kubwa ktk ndoa yangu
 
ish
Kuwa mpole fanya yako.Punguza uchoyo na epuka uvivu

Sent from my SM-J110H using JamiiForums mobile app
u ni kuwa unapokua umeshazoea kuishi kwako unakua na life style yako sasa unapokwenda sasa ukweni unatakiwa uanze kujitune upya nikiwa kwangu ninamaamuzi kuwa leo ni week end sipiki nataka kulala tuu hadi saa tatu sasa upo na wakwe utakuta watu wanaangali saa na kujiuliza hee fulani hadi saa hizi kalala yaani wanaume mnaona ni ishu ndogo lakini kwa ss wanawake kukaliana pamoja ni changamoto
 
mwambie mtafute nyumba ya gharama ndogo kuliko hiyo mnayoishi, mkihamia kwao gharama za maisha za kila siku zitaongeza mara nyingi ataachiwa atoe matumizi yeye kiafrika ukioa tu wanahisi una uwezo, nunua mchele kilo mia na mahindi kilo mia weka ndani mafuta ya alizeti dumi nne za mwaka mzima
 
Ulishakubali kuolewa na
Ukubali tu kuish tu, ukweni
Maana maisha n mlima
Na mabonde kuna kupanda na kushuka ndoa n kuvumiliana

Lakin kuish ukwen aisee
Haa haa kunahitaj
Uvumilivu co wa nchii maana
Kushera jiko na mawifi zako
Mhhh n kubaya aiseee

[Color= yellow]Triple A[/color]
 
KWA KWELI YAANI NITAKONDA NIWE KAMA MOJA
 
.daaah mkuu kwa mwanaume kuishi ukweni ni tusi kubwa kwa sie ole laigwanan ni bora kupambana kuliko kurudisha mpira kwa kipa

Sent from my TECNO-Y6 using JamiiForums mobile app
 
Hiyo miaka minne ungempa saporti mume wako mngekuwa kwenu
ngoja ukaonje joto ya mawe;
YAANI SAPOTI NILIYOITOA HUWEZI KUIJUA WEWE NDUGU YANGU HIYO NYUMBA NI ALIIJENGA YEYE AKAMWAMBIA AHAMIE MAMA YAKE KUMSITIRI KWA KUA HATA WAKATI HUO MAMA AKE ALIKUA ANAISHI KWENYE NYUMBA YA KUPANGA KWA HIYO AKAONA NI VEMA KUMUWEKA MAMA PAZURI NA AKISHATULIA MAMA TUNAANZA KUJENGA KWETU NI MWAKA UNAKARIBIA SASA NA HIYO NI SUCRIFICE NA SUPPORT KUBWA NILIYOKUBALI KUWA MUME WANGU AMUWEKE MAMA KTK MAISHA MAZURI. NA MM NILIKUA COMFORTABLE HAPA TULIPO
 
.daaah mkuu kwa mwanaume kuishi ukweni ni tusi kubwa kwa sie ole laigwanan ni bora kupambana kuliko kurudisha mpira kwa kipa

Sent from my TECNO-Y6 using JamiiForums mobile app
Ni nyumba ya kwake mwanamme lakini alimuweka mama
 
Wewe ni muolewaji utabaki kuwa muolewaji sana sana utaenda kuishi kwa kuigiza no one is perfect ila mapungufu yako ndio itakuwa fimbo ya kuchapwa nayo, Kaa na mumeo mpange mipango yenu kama issue ni kipato ujue utamsadiaje ili kuepukana na issue ya kwenda kuhamia ukweni na huu ndio wakati wa wewe kuwa na msaada mkubwa kwa mumeo, huwenda mumeo anajambo zito linalomsumbua ila anashindwa kukuelezea ukweli kuhusu kipato chake huwenda anaogopa kuaibika mbele yako, pambana ujue anatatizo gani maana hayo sio maamuz ya kiume anayotaka kuyafanya.
 
MBONA WAARABU,WAZUNGU,WACHINA NA WAPEMBA WANAISHI NA WAKWE ZAO AU WEWE MVIVU MVIVU UNANAVYO ONEKANA NDIO MAANA UNAJICONFESS KWA KUHOFIA KUWA UTASHINDWA KUISHI UKWENI
 
Hiyo miaka minne ungempa saporti mume wako mngekuwa kwenu
ngoja ukaonje joto ya mawe;
Ukweli mchungu, aadhani hili pia ni jibu maana huenda dada hakuwa anampa support mme wake. Kama wote mnafaanya kazi hamuwezi kushindwa kulipia hilo pango ila kwa vile dada hapo pengine anamwachia kaka issue nyingi. Kama wadau walivyosema, jaribuni kutafuta nyumba yenye kodi ya chini mhame hiyo ya sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…