Naomba ufafanuzi hili la kuambiwa nianzie Hospitali ya Rufaa

Naomba ufafanuzi hili la kuambiwa nianzie Hospitali ya Rufaa

drilling

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2016
Posts
4,761
Reaction score
4,926
naomba kuuliza wanaojua nina bima ya afya nimekata march 2023 sh 980000/ sijaitumia mpaka hivi leo mwezi huu wa 9 unaingia.

Nimeenda hospital ya CCBRT kumuona daktari wa mifupa na bima yangu wamenikatalia kumuona mpaka nilete referral namba nawaambia mimi sina hiyo referall namba nataka kumuona daktari wa mifupa wamenikatalia kabisa mpaka niipate hiyo referall namba kutoka hospital nyingi.

Hii imekaaje nimeshindwa kumuona daktari wa mifupa ccbrt mpaka niwe na hiyo kwani nimakosa kwenda direct ccbrt kutibiwa mpaka nianzie sehemu nyingine kutibiwa, wahusika nawauliza nijue hii bima yangu itaisha bila kuchekiwa na kutibiwa maumivu yangu
 
Tafuta hosp hapo jilani wakuandikie kufaulishwa kwenda kwao ili upate matibabu!

Au nenda MoI ukapate huduma bila iyo mambo
 
naomba kuuliza wanaojua nina bima ya afya nimekata march 2023 sh 980000/ sijaitumia mpaka hivi leo mwezi huu wa 9 unaingia. nimeenda hospital ya ccbrt kumuona...
Nenda hospita ambayo chini kwa level

Akuandikia referral kwenda huko
Ilitakiwa wakupe maelezo hapo ccbrt
Sema tz seheme nyingi nyingi customer care zero

Ukienda hospital ya chini kingazi

Dr anakuandikia maelezo uende reception ya hiyo hospital wakupe hiyo referral no
Mfano kwa case ya mifupa ungeweza andikiwa hiv

1 .referral to ccbrt
2 code M 15.4
3. Reason for referral . Consultation by orthopedic specialist doctor

Then ukipeleka haya maelezo reception ya hiyo hospita iliyo ngazi ya chini , unapewa referral no cambayo ukienda nayo ccbrt unapokelewa vizuri


Note - ukipata referral no hakikisha unapeleka siku hiyo hiyo sababu tarehe ikibadirika ina expire
 
naomba kuuliza wanaojua nina bima ya afya nimekata march 2023 sh 980000/ sijaitumia mpaka hivi leo mwezi huu wa 9 unaingia. nimeenda hospital ya ccbrt kumuona daktari wa mifupa...
Kwanza mantiki ya Bima si lazima uhakikishe imetumika baada ya kukata. Ni kama vile umekata bima ya gari, nitashangaa sana ukiuliza kwanini usipate faida yake ndani ya kipindi husika maana itaisha kabla hujapata ajali.

Pili, inaonesha wewe una bima ya kifurushi ndio maana unaombwa referral number. Kwa sasa NHIF utaratibu wao ni kwa mgonjwa kupewa referral number toka hospitali ya level ya chini wanapompa rufaa kwenda hospitali kubwa.

Tena waweza pia pewa referral number na hospitali ya chini na bado NHIF wakagoma usihudumiwe hospitali ya juu, ikiwa wanaamini huduma unazotafuta, bado waweza pata hospitali za level ya chini.
 
naomba kuuliza wanaojua nina bima ya afya nimekata march 2023 sh 980000/ sijaitumia mpaka hivi leo mwezi huu wa 9 unaingia. nimeenda hospital ya ccbrt kumuona daktari ...
Nenda hospita ambayo chini kwa level

Akuandikia referral kwenda huko
Ilitakiwa wakupe maelezo hapo ccbrt
Sema tz seheme nyingi nyingi customer care zero

Ukienda hospital ya chini kingazi

Dr anakuandikia maelezo uende reception ya hiyo hospital wakupe hiyo referral no
Mfano kwa case ya mifupa ungeweza andikiwa hiv

1 .referral to ccbrt
2 code M 15.4
3. Reason for referral . Consultation by orthopedic specialist doctor

Then ukipeleka haya maelezo reception ya hiyo hospita iliyo ngazi ya chini , unapewa referral no cambayo ukienda nayo ccbrt unapokelewa vizuri


Note ukipata referral no hakikicha unapeleka siku hiyo hiyo sababu tarehe ikibadirika exipire
 
Bima zina level ww nenda hospitali ngazi ya wilaya kama upo Dar Mwananyamala , Temeke nenda hizo alafu fata maelekezo ya mdau juu hapo
 
Back
Top Bottom