Naomba ufafanuzi juu ya dose sa metakelfin kwa ajili ya kujikinga na malaria

Chilisosi

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2008
Posts
3,050
Reaction score
747
Wana jamvi.

Mimi ni muoga sana wa malaria na ni ugonjwa ambao huwa unanionea sana, Hi imenifanya kila nikija kutembea nyumbani lazima ninywe full dose ya metakelfin kama kinga, huwa nakunywa vidonge vitatu na baada ya wiki narudia vitatu.

Wiki iliyopita nilisafiri tena kuja nyumbani na na Kenya , na nilipokuwa nanunua dawa Nairobi yule muuzaji akaniambia nahitaji vitatu tu sio zaidi lakini kwa sababu nimezoea kubwia mara mbili nikanunua sita.

Mimi nawaomba washauri hapa jamvini wanipe ushauri.

Je ni lazima ninywe mara mbili hizi metakelfin kama kinga?

Na nikiugua je inakuwaje manake nimezoea kunywa kila baada ya miezi sita nilipokuwa naishi Nyumbani lakini toka nihamie UK nimeacha kunywa kwa sababu huku hakuna mbu.

Naomba ushauri tu jamani tuweke hizi siasa pembeni tushauriane kama ndugu hapa please

Ahsanteni
cc MziziMkavu
 
Acha kunywa kama kinga.....subiri muda wa kurudi uk ukikaribia nenda kapime kisha wakikuona una vidudu uanze dose ukifika tu uk ....au unaweza kununua dawa zako then ukifika uk unaanza dose .....mi ndio nnavyofanya miaka yote
 
Mkuu sawa lakini hiyo dose ni vitatu au sita? I mean mara moja au kurudia?
 
Kuhusu dawa kwa kweli sina uzoefu nazo...maana mi huwa naulizaga the best one kisha nanunua .....ila zipo za kumeza kwa siku moja tu ....tusubiri wenye kuzijua watutajie majina
 
Ni vitatu tu na ni mara moja tu hiyo ndiyo dozi ninayoijua tangu nilipozifahamu metacalfin hadi hivi leo.
 
Ni vitatu tu na ni mara moja tu hiyo ndiyo dozi ninayoijua tangu nilipozifahamu metacalfin hadi hivi leo.
Na ni baada ya siku ngappi naruhusiwa kuanza kupata kilaji?
 
Kabla ya kumeza pima kwanza uzito wako kuanzia kilo 80 unaweza 3 chini ya hapo unameza 2.

Unameza dawa za malaria bila kuugua malaria kamanda?
 
Kabla ya kumeza pima kwanza uzito wako kuanzia kilo 80 unaweza 3 chini ya hapo unameza 2.

Unameza dawa za malaria bila kuugua malaria kamanda?
Mkuu nilikuwa Kenya na Bongo wiki iliyopita na ninajua lazima mbu walipitia si unajua tena huwezi kumkwepa mbu na dawa ni kumeza kinga kabla sijaanza kusikia baridi manake huku malaria hawaijui vizuri, wanaweza kuzani mafua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…