Naomba Ufafanuzi juu ya elimu ya VETA

mr planB

Member
Joined
Jun 11, 2014
Posts
15
Reaction score
1
Habarini wana jamvi.

Ndugu zangu kwa yeyote anaejua juu ya elimu/taaluma inayotolewa na hivi vio vyetu vya ufundi stadi/veta nilikuwa naomba anisahidie katika hili na ikiwezekana achimbe ndani zaidi,

Muhitimu wa veta anatambulika ktk soko la ajira?

kunauwezekano wa kuendelea na elimu ya juu kwa kupitia veta?

Ahsanteni natumaini kupata ufafanuzi mzuri .
 
Anaweza kuendelea na elimu ya juu kama DIT
 
Muhitimu wa Veta anatambulika ktk soko la ajira. Na anaweza kuendelea na elimu ya juu akiwa na sifa Za kuingilia means that matokeo ya kidato cha nne au sita yanahusika.

Kwa mwenye cheti cha ufundi level 1 na 2 dhamani trade test grade 3 na 2 cheo chake ni fundi sanifu msaidizi. Kwa mwenye nta level 3 au trade grade one cheo chake ni fundi sanifu daraja la pili kwa mujibu wa kanuni Za utumishi nchini Tanzania na wanaajiriwa serikalini mashirika ya uma na makampuni binafsi na kujiajiri pia.

Wenye grade One au level 3 plus matokeo mazuri ya kidato cha nne au sita anaweza kujiunga na elimu ya diploma katika vyuo vya Arusha technical college ATC. Dar institute of science and technology DIT. St Joseph engineering college. na Mbeya university of science and technology MUST zamani MTC. MIST. Na sasa MUST. hatimaye bachelor masters phd hadi prof.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…