Naomba ufafanuzi juu ya kifaa cha microchip

Mkuu Eiyer yawezekana wengi hatuelewi kwa haya mambo ya microchip na namba 666 ndio maana tumekuwa waamini wa kile tunachopotoshwa.

Sasa nimekuelewa!
Ni kweli mkuu watu wanapotosha kwa makusudi au kwa kutokujua....

Masuala ya unabii huu wa siku za mwisho unazidi kuwa rahisi kadiri tunavyokaribia...

Miaka ya 1500 huko walidhania mengi kuhusiana na unabii huu lakini hawakuwa sawa,imeendelea hivyo lakini leo hii mambo yanazidi kufunguka tu na ndiyo maana Danieli aliambiwa kuwa ayafunge maana ni ya wakati ujao,inawezekana tunaukaribia sana ndiyo maana watu wanaanza kuhisi hisi zaidi na kwa wingi lakini tuache maandiko yajifunue yenyewe....

Tufuatilie sana matukio yanayoendelea kutokea duniani na kusoma sana maandiko matakatifu yanayohusu unabii wa siku hizi ili tuweze kuelewa na kuepuka kupotoshwa kirahisi....
 
Dah!
Nashukuru nilijitoa kwenye mambo ya dini, uongo mwingi, complications kibao, mtu unaishi huna furaha hata kidogo.
Hakuna kitu kama micro-chip wala 666 wala mnyama wala mauzauza mengine. Em ishi kwa amani, fanya kazi, piga hela, kula bata, zunguka dunia, tenda mema. Achana na presha presha, itafika siku yako utakufa, story imeishia hapo.
I'm sorry kama naingilia imani yako ila dini ni ujinga mtupu.
 
Microchip ni kipande kidogo Chenye madini ya Silicon ambacho kiko programmed kufanya instructions fulani
 
ni kweli kbs ila mada ni ndefu sn kuelezea ila vinahusiano wa moja kwa moja
 
google ficarius filii dei una ufahamu ila bado unahitaji kujua zaidi?soma daniel na ufunuo vzr sifa za mnyama zipo wazi na mnyama yupo toka zmn sn na ana sifa tajwa kwenye biblia
 
Na kwa wasiojua vitambulisho vya taifa hivi vya NIDA kitabeba. Nafasi za vitambulisho vyoote mfano ATM card, Leseni ya Udereva, Kadi ya Bima, Kitambulisho cha kazi/ shule, passport na kadha wa kadha.

Hapo hiyo microchip itakuja kurahisisha tu maisha, maana vitambulisho hupotea hivyo wao watasema ni maendeleo ya teknolojia kwamba tuweke hiyo chip kwenye mikono so ukienda bank au popote pale kutakuwa na ile mashine ya kukutambua kwa taarifa zako zilizo ktk chip. Itatambuliwa kwa kumulokwa na kile kifaa cha kusomea barcode kama vya supermarket au ferry ukiwa waboard boti.

Ila sababu mbalimbali aidha ajali na watu wengine hawatokuwa na mikoni hivyo ndipo hako kachip katawekwa kwenye paji la uso. Maana waweza kosa mkono na ukaishi ila si kichwa.

Hapo ndipo Ufunuo wa Yohana unapoenda kutimia.

Chip chapa ila inakwenda facilitate chapa ya mnyama.

Hapo ndio watakao kataa kuikubali chapa ya mnyama basi chip zao huzimwa au hufutwa. ndipo watakapo enda bank au hospitali au madukani hawatoweza pata huduma sababu chip zao zitakufa offline hivyo hawatotambulika.

Kutotambulika huko ndio kusihindwa nunia au uza.
 
google ficarius filii dei una ufahamu ila bado unahitaji kujua zaidi?soma daniel na ufunuo vzr sifa za mnyama zipo wazi na mnyama yupo toka zmn sn na ana sifa tajwa kwenye biblia
Dah!!

Wewe jamaa una mawazo ya kizamani san ambayo tayari yameshashindwa vibaya sana kutokana na mawazo hayo kuwa kinyume na unabii...

Kwa anayejua akisoma hayo maelezo yangu atajua kuwa sijaandika kitu kwa kubahatisha au mtu asiyejua maandiko,lakini wewe umeshindwa kujua hilo na umekuja speed na kuniambia nisome Danieli na Ufunuo utadhani unaniambia kitu kiipya wakati hicho unachotaka nisome nakijua sana tu....

Labda tu nikuambie kuwa nafahamu sana kuhusu unabii wa Danieli 7,2,8,10,11 na 12 kuliko unavyodhani wewe,nafahamu kuhusu Ufunuo kuliko unavyodhani wewe,nafahamu kuwa unabii wa ziku za mwisho haujaandikwa kwenye vitabu hivyo pekee bali umeandikwa pia kwenye Ezekieli,Mika,Isaya,Yeremia n.k,sasa wewe umekariri Ufunuo na Danieli tu....

Kote huko huo unabii unaousema wewe umeshindwa vibaya sana...

Unaniambia ni google Vicarius Filii Dei,yaani nimecheka,eti ni google,hiki unachoniambia nakijua vizurisana tena sana tu,labda nikuulize,Vicarius Filii Dei [Vicar of son of God] ni jina la nani? Nikutahadharishe tu kuwa kuwa makini unapojibu hili swali maana majibu yake yatakukwama kooni....

Kwa kifupi sijaona kipya bali unaniletea hadithi za kizamani ambazo zimeshagaragazwa na unabii siku nyingi tu.....
 
Sasa hiyo chip inakuwaje chapa ya mnyama?

Na ni mnyama yupi huyo?
 
Umefundishwa kupinga ni sawa kwako ningekusaidia ila ni uvivu kumsaidia mtu mwenye akili mgando
 
Umefundishwa kupinga ni sawa kwako ningekusaidia ila ni uvivu kumsaidia mtu mwenye akili mgando
Wala hata sishangai wewe kujibu namna hii maana nilijua tu huna majibu....

Umefanya uamuzi bora kabisa kuachana na suala hili....

Hongera sana....
 
Sasa hiyo chip inakuwaje chapa ya mnyama?

Na ni mnyama yupi huyo?
Nikipata wasaa ntaeleza vyema. Ila fahamu vyote tuvifanyavyo sasa ni juhudi za kufanikisha utimilifu wa ufunuo.
 
Nikipata wasaa ntaeleza vyema. Ila fahamu vyote tuvifanyavyo sasa ni juhudi za kufanikisha utimilifu wa ufunuo.
Hilo nalijua sana tu isipokuwa hayo maswali niliyokuuliza.....

Nasubiri huo ufafanuzi wako.....
 
exactly.
 
UFUNUO WA YOHANA 13:1…… .. Soma hapo utaelewa nini maana ya microchip
 

Nakusoma mdogo mdogo hahahahah

siku ya mwisho mambo mengi yatatokea lakini mwisho ule bado!!!!
 
Umefundishwa kupinga ni sawa kwako ningekusaidia ila ni uvivu kumsaidia mtu mwenye akili mgando
Mkuu tulia ulambe dawa.
Huenda ww umefundishwa kutetea ama ku google.
Haya lete basi hicho ulichofundishwa tufaidike sote..
Manake umepingwa kwa hoja na ukasepa kwa staili ya ajabu.
utamsaidiaje mtu wakati unamwambia aende google?
Ww ndo unamsaidia au ni google ndo inamsaidia?
Yeye kasema anachokielewa na ww andika unachofahamu kuhusiana hilo uliloelekeza.
ujue uzuri wa kitu ili ukielezee vizuri/ukipinge vizuri basi uwe unakijua kwa maana ya kukielewa.
Binafs nimemwelewa alivyoelezea ...ningefurahi zaidi tuelewe pia kile unachokielewa ww.
 
Ni mambo ya kizushi ya Kisabato....
 
Hayo mambo wanayo Wasabato, na Walokole wajinga wajinga..
 
k
Sasa hiyo chip inakuwaje chapa ya mnyama?

Na ni mnyama yupi huyo?
wani wewe ulivyosema mnyama hawezi kutanguliwa na chip kwenye comment yako ulikuwa unmaanisha mnyama yupi?
Hivi microchip haiwezi tangulia na kuandaa mazingira ya huo ufalme/mnyama?
 
k

wani wewe ulivyosema mnyama hawezi kutanguliwa na chip kwenye comment yako ulikuwa unmaanisha mnyama yupi?
Hivi microchip haiwezi tangulia na kuandaa mazingira ya huo ufalme/mnyama?
Watu hawajui maudhui ya kitabu cha Ufunuo..matokeo yake wanafananisha vitu vilivyotajjwa na mambo ya ajabu ajabu...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…