Habari ya leo kaka na dada zangu mlio ndani ya jukwaa hili la sheria, mimi ninahitaji ufafanuzi na ushauri iwezekanavyo, juu na tofauti ya majina katika vyeti viwili ambavyo vinakuwa ni vya mtu mmoja.
mimi ninasoma Korea Kusini, Undergraduate yangu nimesoma UDOM na nilikuwa natumia majina mawili (LEONARD Raphael) ambayo pia ni majina ambayo nimekuwa nikitumia secondari, lakini wakati naomba scholarship, application form yangu ya chuo ilinitaka nitumie majina kama yanavyoonekana katika Passport yangu ya kusafiria ambayo ina majina matatu (TILUHONGELWA Raphael Leonard) pia ndo majina yanayoonekana katika cheti changu cha kuzaliwa.
Tofauti iliyopo hapa ni kuongezeka kwa jina la tatu katika cheti changu cha Masters ambacho kitakuwa tofauti na cheti cha Undergraduate.
Kutokana na hili naomba ufafanuzi, Je kutokana na tofauti hii yaweza kuniletea matatizo nimalizapo masomo yangu huku nirudipo Tanzania hasa katika utafutaji wangu wa ajira?, na kama inaonekana kutokukubalika kisheria, kunaumuhimu wa mimi kupata kiapo cha Kisheria (mahakama/wakiri) ili kuweza kuthibitisha kuwa vyeti vyote vihili ni vya mtu mmoja? na kama nitatakiwa niwe na kiapo hicho cha kisheria, nitatakiwa katika kila maombi yangu ya ajira niambatanishe kiapo hicho?
au ninatakiwa nifanye jitihada zingine za kufanya vyeti vyote viwili viwe na majina yanayofanana either majina mawili kama kilivyo cha UDOM ama majina matatu kama kilivyo cha Masters?