Habari za muda huu wakuu ninaomba msaada wa kutaka kujua sheria inasemaje endapo shahidi atataka ,kudhamiria kuharibu au kukwepa ushahidi wa kesi Fulani.
Kama nikimpeleka mtu mahakamani na nikamtaja mtu Fulani ni shahidi wa hiZo tuhuma na akakwepa kutoa ushahid je kuna sheria inayoadhibu juu kosa la kuvuruga ushahidi?
Ndio, sheria ya kanuni za adhabu sura namba 16 katika kifungu chake cha 109 imeweka kosa la kuaribu ushahidi kwa maksudi kabisa ni kosa la jinai na mtu atakae tiwa hatiani anaweza kufungwa mpaka saba.