Naomba ufafanuzi katika hili la Torques vs Horse Power

Okay. Thanks. Nitaongeza juhudi za kuseach petrol cars zaidi.
 
Nina rafiki yangu walimuwekea mafuta machafu kwenye Ford Ranger, katumia 7m kubadili injectors. Tena ni refurbished injectors.
Ilishawahi tokea hili pia.

Kuna wakati tulienda kigoma kikazi, tukaweka mafuta kumbe yamechanganywa na mafuta ya taa.

Gari ikafa ikabidi ibebwe kurudishwa dar, iligharimu almost 5M kurekebisha kila kitu.

Ilikuwa Land Cruiser.
 
Nina rafiki yangu walimuwekea mafuta machafu kwenye Ford Ranger, katumia 7m kubadili injectors. Tena ni refurbished injectors.
Hii kuna jamaa aliweka mafuta ya kupimwa kutoka kwenye tanki la lori kwa kuuziwa bei ndogo na dereva. Gari ilikuwa ni Discovery 3 baada ya muda mfupi gari ikawa inasumbua sana.

Gari ilikuwa mkoani ikabidi ipakiwe kwenye lori iende Dar kurekebishwa.
 
Nadhani hoja ya kuwa na Diesel safi Europe ndo inawapa ujasiri wa kuzimiliki.

Nna jamaa angu ana Benzi GLS mpya kabisa Diesel, namuonea huruma anavyochagua vituo vya mafuta. Anaweza safiri hata km 70 kufuata diesel toka Puma au Total.
 
Gari za diesel za kisasa hata iwe ya Japan inabidi uwe mtu makini kwenye uwekaji mafuta kabla hujajuta.

Mafuta ya kidebe hata ukikuta Lita ni sh 1000 waachie wenye gari za miaka ya 90.

Ndio maana kwangu mimi 1HZ ndio injini bora hata uweke mafuta ya kidebe itamiss kisha utaendelea na safari.
 
Nadhani hoja ya kuwa na Diesel safi Europe ndo inawapa ujasiri wa kuzimiliki.

Nna jamaa angu ana Benzi GLS mpya kabisa Diesel, namuonea huruma anavyochagua vituo vya mafuta. Anaweza safiri hata km 70 kufuata diesel toka Puma au Total.
Lazima afanye hivyo vinginevyo itamcost.
 
Nakumbuka kipindi uchakachuaji umekolea gari zilikufa nozzles balaa hasa vvti na d4 za kijapani. Ndio ilikuwa mwanzo wa mafuta ya taa kupanda bei na uchakachuaji kuisha.
 
Nakumbuka Prado 1kd nazo mafuta machafu kidogo unanunua injectors! Tushazipeleka sana kwaw jamaa mmoja kule Mabibo amarekebisha injectors.
 
Nakumbuka kipindi uchakachuaji umekolea gari zilikufa nozzles balaa hasa vvti na d4 za kijapani. Ndio ilikuwa mwanzo wa mafuta ya taa kupanda bei na uchakachuaji kuisha.
Saizi mikoani watu wenye gari za mjapani hasa Prado na Hilux wanaweka mafuta ya kidebe. Baada ya muda mfupi gari zinaua nozzle wengine mpaka pump.
 
Daa! Umeelezea vizuri saana aise. Safi sana.

Pia huko parts zinapatikana kirahisi, magari wananunua mapya so kwa kiwango kikubwa yanakuwa bado safi na pia yanakuwa bado ndani ya warant. So gharama zinakuwa chini kidogo. Ila hata wao hawashauri kununua diesels zikiwa used. Mwisho suala la uchakachuaji wa mafuta huko chini kidogo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…