Naomba ufafanuzi katika tatizo la Hand break ya gari kung'ang'ania

Naomba ufafanuzi katika tatizo la Hand break ya gari kung'ang'ania

trplmike

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2012
Posts
701
Reaction score
777
Hii issue imenitokea mara mbili.

Mara ya kwanza nilikuwa naendesha gari Pasaka kwenye mvua na tope kali sana. Ile gari baada ya Pasaka nili ipark kama wiki moja hvi bila kuiendesha. Siku natoka gari haisogei mbele wala nyuma.. nilihangaika nayo mbele nyuma kama dakika 15 hvi.. nikasikia imepiga kama kishindo fulani hivi ikaachia.

Baadae kuna gari nyingine tena niliendesha kipindi cha mvua. Niliipark kama siku 4 hivi.. Hii Hand break ilikamata mpaka akaja fundi kufungua na kurudisha.

Baadhi ya watalaamu wakanishauri kama umeendesha gari kwenye mvua na matope na unategemea kuipark muda mrefu.. ni bora usipandishe hand Break.

Wadau kuna ambaye alishakutana na hii kadhia?
 
Thanks and well noted
Hii hata mie imenitokea....ilikaribia kuunguza clutch plate...fundi alikuja kugundua diffu ndo imengangania...ikaendeshwa kwa nguvu pamoja na kusukumwa ikaachia.....ikikaa zaidi ya siku 2 bila kuendeshwa inangangania kwa kiasi.
 
mi nasubiri wataalam waje nipate majibu ya kina.
manake ukisema brake shoe zina ng'ang'ania kwenye drum lazima kuna sababu.
sasa hizo sababu ni zipi hasa ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom