Naomba ufafanuzi kuhusu Distance University

Naomba ufafanuzi kuhusu Distance University

Abby12

Member
Joined
Apr 23, 2022
Posts
24
Reaction score
26
Habari Wadau

Kwa wale wenye uelewa au ambao washawahi kusoma distance learning nahitaji kupata maelezo kidogo kuhusu hichi chuo cha University of People cha America na pengine yupo ambae ashawahi kusoma na labda kutambulika kwake kwa Tanzania na TCU ,Naamini tutafaidika sote kwa mawazo yenu.

Asanteni
 
Maelezo ya Chuo yanapatikana kwenye website yao, ndio maana mnatakiwa mfanye mtihani wa Kingereza, hili si la kuuliza.
 
Maelezo ya Chuo yanapatikana kwenye website yao, ndio maana mnatakiwa mfanye mtihani wa Kingereza, hili si la kuuliza.
Na hilo pia sio jibu sio kila mwenye kuuliza hajui kiengereza muda mwengine kuuliza kunazaa matunda na faida kwa watu wengine ambao hawana ufahamu kuhusu kitu fulani.

Beside ya hicho kiengereza unaweza kusoma kiswahili ambacho ndo lugha yako na baadhi ya sehemu ukataka ufahamu zaidi kutoka kwa wengine au mawazo coz binadamu hatuna ufahamu wa sawa wote
 
Hicho chuo kinatambulika dunia nzima.

Na kinatoa elimu bure, yaani hulipi hata mia.

We andaa tu laptop na bando LA kutosha.
 
Pia vyuo kama hivyo haviitwi Distance University, vinaitwa:

ODL=OPEN AND DISTANCE LEARNING.
 
Maelezo ya Chuo yanapatikana kwenye website yao, ndio maana mnatakiwa mfanye mtihani wa Kingereza, hili si la kuuliza.
Hujajibu swali lake...kama hujaelewa haikuwa na haja kujibu mkuu.
 
Hicho chuo kinatambulika dunia nzima.

Na kinatoa elimu bure, yaani hulipi hata mia.

We andaa tu laptop na bando LA kutosha.
Kwa Tanzania yetu ni muhimu kujiridhisha na tcu kwani hawatabiriki usije unaonekana umetwanga maji kwenye kinu. Kuna mfano wa diploma za ncc education na top up degree ya university of central lancashire ukipeleka cheti nacte au tcu wana downgrade but the rest of the world wanatambua (labda kama wamebadilika).
 
Samahani mkuu unapo semawana downgrade una maanisha ?
 
Samahani mkuu unapo semawana downgrade una maanisha ?
Hii tuliongelea zamani kidogo kwa sasa sijui hali ikoje. Ina maana ukiwapelekea your top up degree wao wana equate na diploma. Lakini hebu waulize pctl (power computers) kwa sasa watakueleza hali ilivyo. Last year niliona kuna kijana wao alipata degree yao.
 
Back
Top Bottom