Naomba ufafanuzi kuhusu gari aina ya Honda Fit kwa biashara ya usafirishaji wa Uber

Naomba ufafanuzi kuhusu gari aina ya Honda Fit kwa biashara ya usafirishaji wa Uber

Jum Records

JF-Expert Member
Joined
Jun 30, 2014
Posts
547
Reaction score
554
Natanguliza shukrani wakuu,

Naomba mnieleweshe kidogo, hivi Gari hizi ndogo (HONDA FIT) zenye ukubwa wa engine 1.3 sawa na (cc 1330) zinaweza kuruhusiwa kufanyiwa biashara ya usafirishaji wa abiria kwa jijini Dsm? maana binafsi nazikubali sana sema sijawah kuziona zikibeba abiria kama Uber je tatizo kubwa ni nini?

Maana nilipitia mitandaoni nikaona zina bei nafuu kidogo dollar CIF 1820 mpaka bandarini lakin naona watu wamekomaa zaidi na gari za Toyota mfano IST, Vitz, Fun cargo nk.

nini kinafanya magari haya ya honda (Honda Fit) yasitumike kibiashara? nikihitaji kununua gari yangu ya honda niifanyie Uber mamlaka zinaruhusu? maana naona Engine zako ni ndogo tu 1.3.

Asanteni naomba mnifumbue macho kidogo.
 
TATIZO letu wabongo tumelogwa na Toyota ndiyo maana tunashindwa kujitanua Kwenye Aina tofauti ya Magari... sikuhizi kuna Aina tofauti Sana ya Magari tofauti na zamani pia Kwa hiyo gari unayoitaka itakufaa Tu Kwenye biashara kitu cha msingi ni kuzingatia Kwanza upatikanaji wa spare parts.

Sikuhizi unaweza kuagiza spare Kwa njia ya mtandao ndiyo maana watu wengi wanajichanganya na michuma ya Aina mbalimbali
 
Natanguliza shukrani wakuu,

Naomba mnieleweshe kidogo, hiv Gari hizi ndogo (HONDA FIT) zenye ukubwa wa engine 1.3 sawa na (cc 1330) model ya mwaka 2005, zinaweza kuruhusiwa kufanyiwa biashara ya usafirishaji wa abiria kwa jijini Dsm? maana binafsi nazikubali sana sema sijawah kuziona zikibeba abiria kama Uber je tatizo kubwa ni nin?

Maana nilipitia mitandaoni nikaona zina bei nafuu kidogo dollar CIF 1820 mpaka bandarini lakin naona watu wamekomaa zaidi na gari za Toyota mfano IST, Vitz, Fun cargo nk.

nin kinafanya magari haya ya honda (Honda Fit) yasitumike kibiashara? nikihitaji kununua gari yangu ya honda niifanyie Uber mamlaka zinaruhusu? maana naona Engine zako ni ndogo tu 1.3

Asanteni naomba mnifumbue macho kidogo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Honda fit biashara ya uber zinafanya bila shida ila kumbuka hapo zamani kdg yapata mwaka sasa uber walitangaza daraja la kawaida mwisho ni gari ya 1300cc na honda fit ina 1330cc
japo naamin wanaweza wasilizuie bora kuuliza
 
Ni gari safi kbsa, kuna 1.3L na 1.5L. Mimi ninayo ya 1.5L, economical fuel consumption na inavumilia shida.
Spares zipo hela yako tuu.
 
Ni gari safi kbsa, kuna 1.3L na 1.5L. Mimi ninayo ya 1.5L, economical fuel consumption na inavumilia shida.
Spares zipo hela yako tuu.
Vipi kwa safari ndefu mkuu, zipo poa? just kwa private safari?
 
Back
Top Bottom