Naomba ufafanuzi kuhusu gari aina ya Toyota Vitz Clavia

kati ya gari nayojutia kuuza ni vitz clavia ,kigari kina roho ya paka ,hakina urafiki na garage mafuta kinanusa nilipiga nacho route za upanga to ununio for five years..... kwa sisi tusiokuwa na pesa za kutosha hii ndio kimbilio letu.

kama mtu anahitaji namshauri anunue tu hatajuta
 
ME MWENYEWE NINALO JUZI KIDOGO NILIUZE NINUNUE NISSANI XTRAIL... JAMAA ALINIPA NISSAN XTRAIL NITEMBELEE KWA WIKI 2 MWANANGU ILINISHINDA IKABIDI NIMWAMBIE ANIRUDISHIE VITZ YANGU...

MASHINE HAINA URAFIKI NA GEREJI WALA HAISUMBUI HUA NAENDA NAYO KUTOKA ARUSHA MWANZA MWANZA TO ARUSHA NA MASHINE INATEMBEA TU BILA SHIDA
 
Kuna mafundi garage wajuaji ... kila kitu huwa wanakikosoa..
Kweli kabisa mkuu. Na unakuta hawajawahi kumiliki hata bajaji zaidi ya kuishia kutengeneza tuu zinapoharibika. Kwakuwa analetewa vitz clavia 3 kwa siku na corola 1, basi anachukulia kuwa vitz zina matatizo sana. Ukiwasikiliza mafundi hautanunua gari kwani kila mmoja anaponda gari iliyomshinda kutengeneza

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Vitz kutoka Mwanza mpaka Arusha?

inawezekana hii mazee?
 

Hivi nikiwa nina 5mil. Cash naweza pata hapa bongo?
 

Nikiwa na 5mil. cash naweza pata gari kama hii kaka? Nina shida sana na usafiri. Nateseka.
Hivi kati ya vitz, passo, starlet unanishauri nitafute gari gani
 
Nashauri ununue vitz iko kisasa kati ya hizo lakini pia inadumu.Tatizo kubwa la hiyo gari ni Sterling rack.
Nikiwa na 5mil. cash naweza pata gari kama hii kaka? Nina shida sana na usafiri. Nateseka.
Hivi kati ya vitz, passo, starlet unanishauri nitafute gari gani
 
Ipo poa mkuu, mi Kuna jamaa yangu anayo mwaka wa tatu anapiga route Dar - Dom kila mwisho mwa juma na safari za Dar - Songea - Mbinga mara kwa mara na haina shida
 
Vitz clavia ni engine ya 2nz yani mfumo wa ist pale mbele wote ndio upo kweny vits clavia ina cc 1290 kiufupi safari ipo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…