Naomba ufafanuzi kuhusu makato ya kodi

Naomba ufafanuzi kuhusu makato ya kodi

Joshua Simon

Member
Joined
Oct 29, 2016
Posts
6
Reaction score
4
Naomba kuelekezwa kama Kuna namna Mimi sielewi.

Ni mara nyingi sana nikikata tiketi ya basi, unakuta kiwango kilichoandikwa pale ni tofauti na kile ulicholipa.

Mfano, nilipanda basi kutoka Mpanda kwenda Dar, nauli ilikua 79,000 kwenye EFD receipt, lakini Mimi nililipa 75,000/=

Kwa uelewa wangu, TRA wanakata mapato kwa % ya EFD sales.

So, kama TRA inakata 10% ya EFD sales, maana huyu alieniuzia risiti atakatwa 7,900 badala ya 7,500 kwa mazingira hayo.

Kwa upande mwingine, binafsi naelewa hakuna mfanyabishashara anaetaka hasara, kwa hiyo siamini kama ni kweli hizi hasara wanazipata kama nilivyoeleza.

Sasa swali langu ni: Je, Kuna uwezekano tunahujumiwa na wafanyabiashara hawa kwamba EFD machine zao hazisomeki kwenye mfumo wa TRA?

Ama Kuna mchezo kati ya TRA na hawa wadau kwa mazingira hayo hayo ya kutuhujumu??
 
Back
Top Bottom