Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu;Salaam wakuu,
Naomba kujua,maziwa ya mbuzi Yana sifa sawa na maziwa ya ngo'mbe?
Nasikia mbuzi wanakuwaga na magonjwa mengi zaidi ya ngo'mbe,Lina ukweli wowote?
Naomba kwa wenye uelewa mnisaidie,maziwa ya mbuzi Yana athari zozote kiafyaaa?
Asante Sana bossMkuu;
1.Maziwa ya mbuzi yana sifa lakini sio sifa sawa na maziwa ya ng'ombe. Maziwa ya mbuzi yana Protein na Butter-fat contents zaidi ya maziwa ya ng'ombe na maji kidogo zaidi ya yale ya ng'ombe.
2."Unasikia...."- maana yake ni Majungu/Uzushi. Halina Ukweli wowote - unless liwe limethibitishwa. Aliyezusha jambo hilo ungelimtaka akutajie japo magonjwa machache. Watu wenye vidonda vya tumbo wanashauriwa watumie Maziwa ya mbuzi kama mojawapo ya Tiba(Remedy).
3. Maziwa hayo kiafya ni mazuri sana. Athari yake ni kwamba Afya yako itaboreka vizuri - sema tu yana ka-harufu fulani hv lakini ukishayazoea utaachana na ya Ng'ombe. Tatizo ni upatikanaji wa maziwa ya mbuzi kutosheleza soko.
NB. Mtembelee Mr. Google kwa uelewa zaidi.